MAPENZI
ya mjini utata mtupu! Ni kauli inayostahili kutumika baada ya
mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Hassan Mobeto kumwaga chozi akidai
kuporwa bwana’ke aliyekuwa akimpa jeuri mjini (jina tunalo) huku zigo la
lawama likimwangukia staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael
‘Lulu’.
Habari
kutoka kwa chanzo makini zilieleza kwamba, kwa sasa kuna bifu jipya
linalotokota mjini likihusisha sakata la Lulu kumpiku Mobeto kwa
bwana’ke aliyekuwa akimgharamia kiasi cha kuwa mwanaume pekee
aliyemwamini hadi kufikia hatua ya kumzalia mtoto.
Ilidaiwa kwamba, jambo hilo Lulu hakulithamini na kuamua kumpiku huku akimuacha akiishia kulalama kila kukicha.
“Najua
hamuujui mchongo huu. Sasa ngoja niwapashe habari kwa kina. Nimeamini
Lulu kweli ni jasiri, maana kwa alichomfanyia Mobeto Mungu ndiye anajua.
PEDESHEE MPYA WA LULU?
“Huwezi kuamini yule bwana wa Mobeto Lulu kaamua kujiweka kwake, inaweza kuwa ngumu watu kukubali lakini ndiyo ukweli wenyewe.
“Unaambiwa
mtiti wa Mobeto na Lulu ulianza kama mwezi mmoja uliopita. Walianza kwa
kuandikana kwa mafumbo kama waimba taarab kwenye mitandao ya kijamii.
MAFUMBO INSTAGRAM
“Nimekutana na rafiki wa Mobeto ndiye kanipa mkanda wote kuwa Lulu
kampiku Mobeto kwa bwana’ke ndiyo maana mafumbo hayaishi Instagram.
MOBETO HATAKI KUMSIKIA LULU
“Kwa sasa Mobeto hataki kusikia habari za Lulu na ukimuuliza anasema
Mungu atamlipia kwani anamshukuru kumtoa huko kwani alipo sasa ana amani
tele,” kilidai chanzo hicho.
MOBETO AFUNGUKA MAZITO
Kwa upande wake, Mobeto alipoulizwa juu ya sakata hilo alisema kuwa kwa
sasa ana mambo yake mengine hivyo habari za Lulu ingekuwa vizuri
akaulizwa yeye na huyo bwana’ke.
Mobeto
alisema kuwa kwa sasa anachoweza kuzungumzia ni juu ya maisha ya mama
yake mzazi na mtoto wake kwani hao ndiyo faraja pekee iliyobaki kwake.
Alisema
kuwa, hapendi kuzungumzia mambo yaliyopita kwani kila jaribu lina
mlango wake wa kutokea hivyo yawezekana yote Mungu aliyapanga akiwa na
sababu za msingi.
“Mambo hayo mimi sitaki hata kuyazungumzia kwa sasa, nafikiri ingekuwa
vyema ukamuuliza Lulu na ….(anamtaja huyo mwanaume) kwani wao ndiyo
wanaweza kukupa ukweli na kukusimulia kiunagaubaga.
MOBETO AMWACHIA MUNGU
“Katika maisha yangu, kwa sasa namwangalia mtoto na mama yangu, hao
wakikosa furaha hata mimi siwezi kuwa na amani kwenye maisha yangu,
kwani mambo mengine yakishapita hakuna sababu ya kuyaendeleza zaidi
namshukuru Mungu.
“Kwa sasa nina michongo yangu mipya na siko tayari tena kuzungumzia habari nje ya familia yangu.
“Ninachoweza
kukuambia ni kwamba maisha yana kila staili ya kuishi hivyo sifikirii
tena kuingia kwenye mitandao ya kijamii kuzungumzia habari za mtu kwani
hata hao wanaonizungumzia sina muda wa kuanza kusoma comments (maoni)
zao wala kuwajibu.
“Kwa
kifupi sijawahi hata kuona mambo yanayozungumzwa kuhusu mimi kwenye
mitandao maana huwa sisomi tena kwani kila mtu ana namna ya maisha
aliyochagua.
“Hata huyo Lulu na timu zake mimi sina muda wa kusoma mambo yao kwani Mungu ndiye tegemeo langu,” alisema Mobeto.
LULU ARUKA MITA MIA
Alipotafutwa Lulu na kupewa taarifa za uporaji wa bwana wa mtu, aliruka
mita mia moja kwa kusema kuwa habari hiyo ni mpya kwake na hajawahi
kusikia lolote ila ndiyo anaambiwa kwa sasa hivyo kama kuna mtu ana
picha zake na huyo bwana wa Mobeto, basi ndiyo anapata taarifa.
“Madai haya kwangu ni mapya na siyajui ndiyo mnaniambia kwa mara ya kwanza, sioni sababu ya kulizungumzia,” alisema Lulu.
chanzo;GPL
Post a Comment