Inawezekana ulikuwa na maswali mengi
kuhusu mipango ya harusi ya staa wa Bongo Fleva Naseeb Abdul aka Diamond
Platnumz na Zari sasa basi ameyajibu kupitia kipindi cha Mseto cha
Citizen kinachoendeshwa na Willy Mtuva.
‘Harusi
haina muda mrefu kwa sababu unajua ndoa inakuwa inapagwa na mwenyezi
Mungu kwa hiyo nisingependa kuzungumza kitu cha uongo, kwanza tulikuwa
tuzae mtoto na hatukutaka kupalamiana kuoana pasipo kujuana kiundani
zaidi kwa hiyo panapomajaliwa nitatangaza rasmi ni lini masuala ya ndoa‘ – Diamond Platnumz
Willy Mtuva:Zari ni mtu maarufu nje ndani ya nyumba yukoje?
‘Yuko
vizuri kwasababu kwanza kikubwa anajua kuna maisha ya umarufu na maisha
ya kutafuta pesa na usipoweza kujiongoza mtu anaweza kutumia pesa vibaya
anajua kwamba ana mwanaume ambaye anahitaji kupikiwa, anatakiwa
kuandaliwa maji na vitu vingine kwa hiyo ni mwanamke anayejitambua’ – Diamond Platnumz
Post a Comment