Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na kumpongeza Nahodha wa Timu ya Taifa Stars, Nadir Haroub
'Canavaro', baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia
kati ya Taifa Stars na Algeria
uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao
ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.
Akizungumza
na wachezaji hao baada ya mchezo huo, Mhe. Samia,aliwataka wachezaji na
viongozi wa Stars kutovunjika moyo kutokana na matokeo ya mchezo huo,
na kuwataka kuongeza juhudi na kujituma zaidi katika mchezo wa marudiano
ili ukweza kupata matokeo mazuri zaidi.
''Japo
mmefungwa lakini tumewaona jinsi mlivyojituma, msivunjike moyo na
matokeo ya mchezo, kwani tumeowana mlivyocheza kwa kujituma, hivyo
naamini hata ugenini mtaweza kupata matokeo mazuri zaidi mkiwa na moyo
huo huo wa utaifa, juhudi na kujituma,
Mtangulizeni
mungu kwa kila jambo na kwa uwezo wake naamini mtaenda kufanya vizuri
katika mchezo wa marudiano, na nawatakieni safari njema leo usiku
kuelekea mchezo huo wa marudiano, sisi wazee wenu na Watanzania wote
tupo nyuma yenu tunawaombe muweze kuwatoa waarabu hawa wenye fitina kali
katika mchezo wa Soka''. alisema Mhe. Samia
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akisalimiana na kumpongeza mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Thomas Ulimwengu,
baada ya mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa
Stars na Algeria uliochezwa jana. Katika
mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias
Maguli na Mbwana Samatta. Kulia ni
Mbwana Samatta, akibugujikwa na machozi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimfariji mchezaji wa Timu ya Taifa Stars, Mbwana Samatta, baada ya mchezo wa
kuwania kufuzu hatua ya makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na
Algeria uliochezwa jana. Baada ya mchezo
huo Samatta, alionekana kubugujikwa na machozi muda wote. Katika mchezo huo
timu hizo zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na
Mbwana Samatta. Picha na www.sufianimafoto.com
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akishangilia sambamba na baadhi ya Viongozi bao la kwanza la Taifa Stars lililofungwa
na Elias Maguli, katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Kuwania kufuzu
hatua ya makundi Kombe la dunia dhidi ya Algeria uliochezwa jana kwenye Uwanja
wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya
2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana Samatta.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza jambo na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamal Malinzi,
wakati walipokuwa Uwanja wa Taifa katika mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya
makundi Kombe la dunia kati ya Taifa Stars na Algeria uliochezwa jana. Katika mchezo huo timu hizo
zilitoka sare ya 2-2, mabao ya Stars yalifungwa na Elias Maguli na Mbwana
Samatta.
Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria mtanange huo jana
Sehemu ya mashabiki waliokuwa Jukwaa kuu
Ila
moja kati ya kituko ilikuwa ni hiki kiti kilichokatika mguu mmoja eti
katika mchezo wa kimataifa kama huu hwakupata kiti chenye hadhi
kulingana na mchezo wenyewe
Timu zikiwa tayari kuanza mtanange huo, hapa zikipigwa nyimbo za taifa
Mudathir Yahya, akiwachora nane waarabu....
Mbwana Samatta, akitesa Waarabu kwa vyenga,akiwageuza atakavyo..
Waarabu waliimarisha ulinzi zaidi kwa Mbwana Samatta.....
Beki wa Stars, Shomari Kapombe, akiruka kwanja la mchezaji wa Algeria
Credit: MichuziJr
Post a Comment