Kwa niaba ya Rais Obama na watu wa Marekani,
nawapongeza watu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uchaguzi wa rais na
wabunge ulioendelea kuthibitisha rekodi nzuri ya Tanzania katika kujenga
demokrasia imara.
Wakati Rais John Pombe Magufuli na
serikali yake wakichukua majukumu yao, tunatarajia kuendelea na ubia wetu wa karibu
na kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya nchi zetu mbili tunapofanya kazi
pamoja ya kusaidia ujenzi wa demokrasia, kukuza usalama wa kikanda na kuendelea
kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Aidha, napenda kumshukuru Rais aliyemaliza
muda wake Jakaya Kikwete kwa jitihada zake za kujenga uhusiano imara na wa
kudumu kati ya Marekani na Tanzania.
Hata
hivyo, Marekani inaendelea kustushwa sana na tamko la mamlaka visiwani Zanzibar
la kusudio la kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar wa Oktoba 25.
Kwa
dhati kabisa, tunatoa wito kwa serikali mpya kuhakikisha kuwa maamuzi ya watu
wa Zanzibar yanajidhihirisha katika
ukamilishwaji wa haraka, wa haki na wa amani wa mchakato wa uchaguzi visiwani
Zanzibar.
Post a Comment