Na Mahmoud Ahmad
[TANZANIA]
Kutoka jiji la Arusha, aliyekuwa mgombea
urais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ADC, Chief
Lutayosa Yemba (Pichani) ametangaza kugombea kiti cha Spika wa bunge la
jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha ADC.
Chief
Yemba, ameyasema hayo leo jijini Arusha, alipokuwa akizungumza na
vyombo vya habari akitoa tathimini ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba
25 mwaka huu, pamoja na kutathimini uchaguzi wa jimbo la Arusha ambao
unatarajiwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu.
Amesema
baada ya kuanguka kwenye urais, sasa anaelekeza nguvu zake kwenye
Usipika, ambako ana uhakika wa kushinda kuwa ana sifa na vigezo na ana
imani atashinda kwa kuwa anaungwa mkono na wabunge wengi wakiwemo wa
CCM.
Aidha,ametumia
fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Arusha kwa kumpigia kura 200 kwenye
uchaguzi mkuu uliopita licha ya chama chake kuwa ni kichanga na sasa
anafanya kazi ya kukijenga mkoani humo.
Amesema
uchaguzi mkuu umekwishana tayari mgombea wa ccm, Dakta John Magufuli,
ndie rais na ADC, inamtambua na inampongeza kwa ushindi huo na hivyo
itashirikiana nae na Pia ADC ingelimtambua mgombea yeyote ambae
angelishinda kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 25 mwaka huu.
Kuhusu
marudio ya uchaguzi wa Zanzibar, Chef Yemba, amesema ADC, itashiriki
kwenye uchaguzi huo ambao ulifutwa kutokana na kugubikwa na kasoro
nyingi na kutabiri kuwa ADC, itakuwa ni sehemu ya serikali ya Zanzibar
kwa kuwa itapata ushindi mkubwa .
Ameiomba
serikali ya mapinduzi Zanzibar, kuvunja tume ya taifa ya uchaguzi na
kuunda nyingine itakayosimamia haki kwa wagombea wote na kuepuka
kasoro zilizojitokeza zisijirudie na kuvuga uchaguzi .
Amesema
kwenye uchaguzi uliopita mawakala wa ADC, walizuiliwa kuingia kwenye
vituo vya uchaguzi kwa ajili ya kuhakiki zoezi zima la uchaguzi mkuu na
kushangazwa na vituko vya matokeo Pemba ambapo yeye Chief Yemba,alipata
kura nyingi zaidi kuliko mgombea urasi wa Zanzibar, Hamad Rashid, ambae
Pemba ndio ngome yake alipata kura 114 lakini ilijaziwa kura 4 wakati
yeye akipata kura 90.
Kuhusu
uchaguzi wa ubunge jimbo la Arusha, ameipa ccm 38% Chadema 30 na ACT
wazalendo 6%, na kusema kuwa huo ni kwa mjibu wa utafiti alioufanya wa
kuzungumza na makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo waztu wazima
vijana na wanawake.
Ameongeza kuwa hata hivyo ushindi utaamuliwa na kundi la waswahili ambalo mpaka sasa halijatoa mwelekeo wa nani wamuunge mkono.
Yemba, amesema ADC katika uchaguzi huo haifungamani na chama chochote bali inahitaji mbunge na sio chama cha siasa .
Amesema
kinachohitaji kwa Arusha ni kupata mbunge bora makini atakaezungumzia
namna ya kuboresha huduma za afya ,elimu na sio kusuguana na serikali
ili Arusha iweze kusonga mbele katika maendeleo.
“Umefika
wakati wanasiasa kuachana na siasa za misuguano kati ya wanasiasa na
viongozi wa serikali ili Arusha iweze kusonga mbele”alisema yemba.
Ameongeza
kuwa mbunge wa Arusha, anayetetea kiti chake ameshindwa kufanya
mabadiliko ya maendeleo na badala yake amejenga chama chake ,wananchi
wanahitaji mbunge wa kuwasemea na sio chama cha mtu.
Yemba,
Amesema ADC,ilikuwa inategemea kuona wananchi wakiandamana kupinga bei
ya maji kupanda licha ya kuandamana kwa ajili ya kukosekana kwa maji
pekee.
Post a Comment