Moja
ya vyama muhimu katika kuleta mapinduzi ya Kilimo Nchini Tanzania ni
Tanzania Agricultural Organisation (TASO). Pamoja na majukumu mengine,
TASO ndio wamiliki na wasimamiaji wamaonyesho ya nanenane Nchini
Tanzania.
Hadi sasa TASO ina viwanja vitano vya maonyesho ya nanenane kwenye kanda za Kaskazini-Arusha, kandayalati –Dodoma, Mashariki – Morogoro, NyandazaJuu –Mbeya na Kanda ya Kusini – Lindi. Mfumo wa utendaji wa TASO umeanzia kwenye Kata, Wilaya, Mkoa, Kanda naTaifa.

Juhudi
zinafanyika kuanzisha viwanja vya maonyesho kwenye kanda ya Magharibi
na kanda ya ziwa katika muda mfupi ujao. Tanzania ikiwa inatumia si
zaidi ya asilia 25% ya Aridhi inayofaa kulimwa, Kilimo kinabakia kuwa
msingi muhimu wa kukuza uchumi na ajira Nchini Tanzania.
Pia izingatiwe kuwa Tanzania ina jumla asilimia 46% ya aridhi yote ya Afrika Mashariki hivyo kuwa na fursa kubwa ya kukuza soko na kulisha nchin yingine za Afrika Mashariki na nje.
Pia izingatiwe kuwa Tanzania ina jumla asilimia 46% ya aridhi yote ya Afrika Mashariki hivyo kuwa na fursa kubwa ya kukuza soko na kulisha nchin yingine za Afrika Mashariki na nje.
Jumamosi
yaTarehe 14 Novemba 2015 mjini Dodoma, TASO ilifanya uchaguzi wa
viongozi wa Taifa ambao wataongoza taasisi hii muhimu katika kukuza
kilimo kwa miaka 5. Viongozi waliochaguliwa ni Engelbert Moyo –
Mwenyekiti, SharifaAbebe – Makamu Mwenyekiti, Imani Kajula – Katibu
Mkuu, Daudi Mwalusyamba – Katibu Mkuu Msaidizi na Michael Lupyana –
Mweka Hazina.
Akizungumza
baada ya kuchaguliw aMwenyekiti wa TASO Taifa Engelbert Moyo alisema ‘’
Huu ni mwanzo mpya wenye malengo ya kuchochea mchango wa kilimo katika
Uchumi, Maisha ya Watanzania, weredi katika kilimo na ajira. Ni fursa
adhimu kuwa na viongozi waTaifa wenye ujuzi katika fani mbalimbali;
Kilimo, Biashara, Masoko naFedha. Naamini kuwa TASO itapiga hatua kubwa
katika kuwa muda muhimu katika kutoa mchango katika sekta hii nyeti’’.
Nae
Katibu Mkuu wa TASO Imani Kajula alisema ‘’ Kilimo ni sekta yenye
kuajiri watanzania wengi, lakini imekuwa na changamoto nyingi,
tunatambua kazi hii tuliyopewa ni adhimu na muhimu katika kuleta
mabadiliko ya kukuza soko la mazao, ubunifu watechnojia rahisi za
kilimo, upatikanaji wa habariza kilimo, uvuvi, ufugaji na masoko kwa
wakulima na pia kuboresha maonyesho ya Nanenane kuwa jukwaa la kuchochea
ukuaji wa kilimo na ajira’’.
Post a Comment