Mhadhiri huyo ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini amezungumza hayo alipokuwa katika mahojiano maalum na Kituo cha Televisheni cha Azam Two muda mfupi jana baada ya kuapishwa kwa Dk. Magufuli.
Dk.
Magufuli ameapishwa leo baada ya kupata ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu
uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu kwa kupata asilimia 58.46.
Amesema
kuwa, Rais Magufuli haanzi kazi mpya bali anaendeleza kazi walizoacha
watangulizi wake kuanzia Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius
Nyerere.
Ameeleza
kwamba miongoni mwa kazi ngumu zinayomkabili ni pamoja na kumaliza
mgogoro kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao unaonekana
kutofika mwisho.
Katika
mahojiano hao amesema, Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete pamoja
na kufanya juhudi zake katika kutatua mgogoro huo, kazi hiyo
hakuimaliza.
Ameeleza
kwamba hakuna sababu ya kushirikisha mataifa ya nje katika kutatua
mzozo wa Zanzibar na kwamba, dukuduku la Muungano linaweza kutatuliwa
ndani ya nchi pekee
Post a Comment