Muhubiri wa kimataifa nabii maarufu duniani Temipote Balogun maarufu kama TB Joshua ameacha maswali baada ya kushindwa kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mpya wa awamu ya tano Dk.John Magufuli.
TB
Joshua aliwasili nchini November 03 kwa ndege binafsi na kupokewa na
Dk.MAGUFULI pamoja na Mbunge mteule Mwigulu Nchemba katika uwanja wa
kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere,Dar es salaam.
Baada
ya kuwasili alifanya mazungumzo ya faragha na Dk.MAGUFULI pamoja na
rais mstaafu Jakaya Kikwete kisha kufanya mazungumzo zaidi ya saa tatu
na Edward Lowassa.
Ujio
wa nabii huyo ulionekana kama amekuja kwa ajili ya kuapishwa kwa
Dk.Magufuli lakini huku baadhi ya wananchi wakifurahishwa na ujio wake
na kuamini ni fursa pekee ya kukutana naye na kufanya maombi akiwa hapa
nchini.
Baadhi
ya watu walisema waliamua kwenda uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kumuona
nabii huyo lakini haikuwa hivyo na hawakufahamu kwa nini hakuhudhuria
sherehe hizo.
Post a Comment