Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

ACT ­ Wazalendo yapata mgombea ubunge Arusha Mjini

Hatimaye Chama cha ACT­Wazalendo mkoani Arusha kimempata mgombea atakayepeperusha bendera yake katika uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini. 

Hatua hiyo imekuja baada ya chama hicho kuhaha kwa siku kadhaa hadi dakika za mwisho kumpata mtu wa kuwania jimbo hilo baada ya uchaguzi kuahirishwa kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea kupitia chama hicho, Estomih Mallah kufariki dunia katikati ya kampeni. 

Katibu wa chama hicho mkoani Arusha, Daniel Olotu alimtaja Navoy Mollel kuwa ndiye mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho baada ya kushinda katika kura za maoni kwa kupata alama 62. 

Olotu alisema mkutano mkuu wa chama hicho ulimpitisha Mollel baada ya kuwashinda wenzake wanane, akifuatiwa na Hagai Mollel aliyepata kura 34 na John Saitabau aliyepata kura 22. 

Uchaguzi huo unafanyika sambamba na majimbo mengine matatu ya Ulanga Mashariki, Handeni Mjini na Ludewa ambako wagombea wa CCM walifariki dunia pamoja na Lushoto ambako mgombea wa Chadema alifariki dunia.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top