Rais
Dkt.John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya
kuwasili katika makao makuu ya Wizara ya Fedha(HAZINA) kwa ziara ya
kushtukiza leo mchana.Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Servacius
Likwelile.Rais Magufuli alitembelea na kukagua ofisi zote wizarani hapo
na kisha kuongea na viongozi waandamizi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli
amefanya ziara ya kushtukiza kwa kutembea kwa miguu kutoka Ikulu hadi
katika Wizara ya Fedha na kukagua utendaji kazi wa wafanyakazi wa ofisi
hizo, hata hivyo alikuta baadhi ya maofisa wakiwa nje ya ofisi zao.
Rais
Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na wafanyakazi wawili wa Wizara ya Fedha
ambao ni walemavu Bwana Fundi Maruma na Frank Mkyama wakati Rais
alipofanya ziara ya kushtukiza wizarani hapo leo.
Rais
Dkt.John Pombe Magufuli akizungumza na viongozi waandamizi wa Wizara ya
Fedha wakati alipofanya ziara ya kushtukiza Wizarani hapo ambapo alitoa
maagizo ya kuziba mianya ya wakwepa kodi.
(Picha na Freddy Maro)
Post a Comment