Baada
ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Star’ kulazimishwa sare ya
kufungana magoli 2-2 na Algeria kwenye uwanja wa taifa, kocha mkuu wa
kikosi hicho Charles Boniface Mkwasa amesema, mabadiliko yaliyofanywa na
benchi la ufundi kumtoa Elius Maguli na kumingiza Mrisho Ngassa
hayakuzaa matunda kama walivyotarajia.
Mkwasa
amesema, walimuanziasha Maguli kwasababu ni mchezaji ambaye anatumia
nguvu na anaweza kupambana kwa kutumia mwili wake lakini baadaye
walimpumzisha wakiamini kuingia kwa Ngassa kungeifanya timu kutengeneza
nafasi nyingi zaidi za kufunga kwasanbabu Ngassa anaspidi na uwezo wa
kutengeneza nafasi.
“Niseme
tu kwamba leo (jana) ilikuwa ni game yetu 100% tumetengeneza nafasi
nyingi sana lakini tumeshindwa kuzitumia tumepata goli mbili lakini kuna
muda tumepoteza concentration wakaweza kurudisha goli zote mbili lakini
vijana wamepambana wamehangaika kutafuta magoli kutokana na nafaisi
zilizopatikana na wakati mwingine tunasema mpira unabahati na Algeria
wanabahati sana”, alisema Mkwasa.
“Vijana
wamejitahidi lakini niseme tulifanya makosa pengine wakati wa kufanya
mabadiliko kwasababu timu ilishakuwa stable lakini ni matokeo ya mchezo
na nafikiri bado tunamlima mrefu kwasababu ninavyowatazama hawa nyumbani
kwao watabadilika. Lakini uwezo wa kuwafunga tunao timu yao sio nzuri
sana kiasi kwamba haifungiki”.
“Niwashukuru
watanzania na waandishi wa habari kwa kuhamasisha na watanzania
wameweza kuitikia na tumeona jinsi gani wameishangilia timu yao lakini
wasife moyo kwa matokeo haya, tupo katika mchakato wa kujenga timu
naamini katika muda mfupi tutakuwa na timu nzuri kama wenzetu ambavyo
wanatimu zao”.
“Niwashukuru
pia wachezaji na wengine wote ambao tumeshirikiana, kamati pamoja na
TFF kwa kuweza kuonesha kiwango ambacho kwa muda mrefu hakijaonekana”.
Kikosi cha Stars kimeondoka jana usiku kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumanne November 17.
Post a Comment