Jeshi
la Polisi linawashikilia watu wanne wanaodaiwa kuhusika na kifo cha
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoani
Geita Alphonce Mawazo.
Kifo
cha marehemu Mawazo kimetokea jumamosi hii Novemba 14 majira ya saa
sita mchana baada ya kuvamiwa na kundi la watu na kuanza kumshambulia
kwa silaha za jadi.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Geita Mponjoli Mwabulambo amesema chanzo cha tukio ni kwamba kulikuwa na
mkutano wa ndani ya chama cha chadema uliofanyika ukumbi wa ludete b
ulikuwa unahusu mambo yao ya uchaguzi na walipokuwa wanaendelea katika
kikao chao kuna mtu ambaye anadaiwa ni mfuasi wa chadema na
kumnong’oneza Marehemu mawazo na baada ya hapo wajumbe walipata mshutuko
na kutoka nje na wakakutana na kundi la watu na mtafaruki ulianzia
hapo.
Ameongeza
kuwa tatizo hilo kutokea kunahusishwa pia na itikadi za kisiasa lakini
bado jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wake.
Hata hivyo Kamanda Mponjoli amesema hali ni nzuri maeneo ya katoro hasa kata ya ludete ambapo uchaguzi wa diwani umefanyika.
1 comments:
Jamani imeniuma sana Mungu amlinde mahari pema pepon AMEN..
ReplyPost a Comment