Jeshi
la Polisi mkoani Kagera limelazimika kutumia nguvu kuwatawanya
wanafunzi zaidi ya mia nane wa kidato cha tano na cha sita katika shule
ya sekondari ya Ihungo waliofanya maandamamo yasiyo rasmi wakati
wakielekea kwa mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Bukoba kwa lengo la
kuelezea matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo shuleni hapo
yanayohusina na masuala ya chakula, afya na taaluma.
Jeshi
la Polisi lililazimika kutumia nguvu za kuwatawanya wanafunzi hao
waliokuwa wakiiba nyimbo mbalimbali huku wapiga kelele baada ya kukaidi
maekezo yaliyokuwa yanatolewa na maofisa wa jeshi hilo yaliyokuwa
yanawataka watawanyike ili matatizo yao yatafutiwe ufumbuzi.
Awali,
wakizungumza wakati wakielezea matatizo yaliyowapekelekea hadi
wakafikia uamzi wa kuchukua hatua ya kuandamana kwa lengo la kuonana na
mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Bukoba wanafunzi hao wameelezea kuwa
wanapewa chakula kisichofaa kwa matumizi ya binadamu na wakati mwingine
wanapewa mulo mmoja au milo miwili badala ya milo mitatu iliyopangwa pia
wamelalamikia hali ya vyoo kwa kusema vinahatarisha afya zao kwa kuwa
ni vibovu na hivyo vinaweza kusababisha mlipuko wa magonjwa.
Naye,
Philip Boneventula mkuu wa shule ya sekondari ya Ihungo akizungumza
amesema malalamiko ya wanafunzi ni ya kweli, amesema tatizo la chakula
linaloikabili shule hiyo linatokana na hatua ya wazabuni ya kusitisha
huduma ya usambazaji wa chakula kufuatia deni kubwa wanalodai shule la
zaidi ya shilingi milioni mia moja kumi na tatu, huku afisa taaluma wa
sekondari katika manispaa ya Bukoba, Wandela Lwakatare kwa niaba ya
mkurugenzi mtendaji wa manispaa ya Bukoba akielezea mambo yanayochangia
matatizo yanayozikumba shule za sekondari za bweni za serikali ambayo
ameyataja kuwa ni pamoja na ucheleweshwaji wa ruzuku.
Post a Comment