Mwili wa mtoto Joseph kama ulivyokutwa kisimani
Mtoto Joseph mwenye umri
wa miaka 7 alikutwa ametupwa katika kisima cha jirani yao usiku wa
kuamkia jumatatu tar.16/11/2015, hapa Yombo vituka maarufu kama kwa
Chande.
Taarifa za wazazi
zinasema mtoto wao walianza kumtafuta usiku saa 2 baada ya kutoonekana
nyumbani. Walitembea na kuuliza kila mahali lakini hakukuwa na taarifa
za kuonekana kwake. Baadae walitoa taarifa za kupotea kwake katika kituo
kidogo cha police Yombo Vituka.
Usiku huo walijaribu
kuangalia katika kisima (ambacho kesho yake alionekana humo) lakini
pamoja na kuingiza mti mrefu na kukoroga kwenye maji hakukuwa na dalili
za kuwemo kiumbe huyo.
Kesho yake Jumatatu tar.
16/10/2015. Saa 12 alfajiri, mtu mmoja aitwae Kilongola ambae ni jirani
alitoa taarifa za kuona kiumbe katika kisima kilekile ambacho
walikiangalia usiku.
Ilikuwa ni simanzi kubwa! Baadae police Chang'ombe waliuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi.
Taarifa zilizopatikana
baada ya uchunguzi wa kitaalamu zilionyesha kabla ya kifo chake marehemu
alilawitiwa kisha kunyongwa na kutupwa katika kisima kile akiwa
amekufa.
Mauaji hayo ya kikatili yanahusishwa na bw.Kilongola ambae ni jirani wa familia hiyo.
Kuna taarifa kwamba
marehemu alikutwa akicheza mchezo usiofaa na binti wa Kilongola mwenye
miaka 5. Tukio hilo lilishuhudiwa na mke wa Kilongola. Mke huyo
hakufurahishwa na kitendo hicho cha Joseph (marehemu) kumfanyia binti
yake. Alimchukua hadi kwa wazazi wake na kuwaeleza kitendo alichokuwa
anafanya mtoto wao kwa bintiye.
Wazazi wa Joseph
walimuadhibu mtoto wao na kumuonya asirudie tena. Waliyazungumza kama
wazazi kisha wakayamaliza. Hiyo ilikuwa Jumamosi tar.14/11/2015.
Bw. Kilongola aliporejea
nyumbani na kuelezwa taarifa za kufanyiwa kitu kibaya mtoto wake,
hazikumfurahisha na kueleza kutoridhishwa na maamuzi waliyofanya na
kusema hayo ni ya kwao yeye atajua cha kufanya.
Kwa sasa bwana Kilongola, mkewe na wazazi wao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi.
Mwili wa marehemu unasafirishwa kwenda kwao Moshi kwa mazishi.
Post a Comment