Mbunge
Mteule wa Jimbo la Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe (pichani) amesema
Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania atatokana na
uteuzi utakaoidhinishwa na Bunge na si taarifa zilizopo sasa katika
mitandao ya kijamii.
Dkt.
Mwakyembe ambaye amewahi kuwa Waziri wa Uchukuzi katika Serikali ya
Awamu ya Nne, alisema kwa mujibu wa sheria na katiba ya nchi, Waziri
Mkuu anateuliwa na Rais ambaye huwasilisha jina hilo kwa Spika wa Bunge
na baadaye kupigiwa kura na Wabunge.
Mbunge
huyo aliyasema hayo jana Jumapili (Novemba 15, 2015) Mjini Dodoma
wakati alipokuwa akihojiwa na vyombo vya habari kuhusu tetesi zilizopo
katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii
kuhusiana na jina lake kutajwa kuwa ndiye Waziri Mkuu wa Serikali ya
Awamu ya Tano.
“Mimi
siwezi kuwasemea wananchi na siwezi kusema kuna watu wengi wanasema
hivi, kwani nafasi ya Uwaziri Mkuu haiji kwa njia ya kura ya maoni,
wala kwa njia ya mitandao ya kijamii ni nafasi ya uteuzi
inayoidhinishwa na bunge na ni mamlaka ya Rais wa nchi” alisema Dkt. Mwakyembe.
Aidha,
Mhe. Mwakyembe aliwataka Watanzania bila kujali itikadi za dini na
vyama vyao wamuombee Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili aweze kuchague
viongozi watakao wajibika na ambao wataendana na kasi ya Mhe. Rais.
Wabunge
wengine waliotajwa kuwepo kwa uwezekano wa kuteuliwa nafasi ya Uwaziri
Mkuu wa Awamu ya Tano ya Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli ni pamoja
na Mhe. William Lukuvi, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo na Mhe. January
Makamba.
Post a Comment