Mwanamke aitwaye, Asma Jama ameshambuliwa nchini Marekani kwa kuongea Kiswahili
Jama alikuwa amekaa na familia yake kwenye mgahawa wa Applebee huko Minnesota, akikata kiu na juice huku
mazungumzo yakiendelea kabla ya kujeruhiwa vibaya mdomoni. Mwanamke aliyekuwa amekaa jirani yake
alimponda na glasi nzito ya bia mdomoni.
Sababu? Jama alikuwa akizungumza Kiswahili na familia yake.
“Siamini baada ya miaka yote hii mtu ananipiga sababu niko tofauti,” alisema Jama. “Mtu ananipiga kwasababu
nilikuwa nikizungumza lugha ya kigeni.”
Shambulio lilimwacha Jama na majeraha usoni pamoja na mdomo kuchanika kiasi cha kushonwa nyuzi 17.
Jodie BurchardRisch, 43, na mume wake, walikuwa wamekaa kwenye mgahawa huo jirani na Jama, aliyekuwa
ameketi na binamu na watoto wa nduguze. Wawili hao walichukizwa baada ya kumsikiliza Jama na familia yake
wakizungumza lugha ngeni.
Jama alisema wawili hao waliwaambia waende nyumbani. “Walisema ukiwa Marekani unatakiwa kuzungumza
Kiingereza.”
Jama, ambaye ni msomali, alihamia Minnesota mwaka 2000 kutoka Kenya. Anazungumza lugha: Kiingereza,
Kiswahili na Kisomali.
Jumatatu hii, BurchardRisch alishikiliwa kwa kosa la shambulio.
Kutokana na shambulio hilo, Jama anadai hana amani tena na anafikiria kuhama Minnesota. Amesema anaweza
kuungana na dada yake aliyehama Minnesota mwezi June na kwenda Dallas.
Post a Comment