Wanajeshi
wastaafu zaidi ya 4000 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania mkoa wa
Morogoro wamelalamikia serikali za awamu zilizopita kuwatelekeza bila
kuwahudumia.
Wanajeshi
wastaafu zaidi ya 4000 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania mkoa wa
Morogoro wamelalamikia serikali za awamu zilizopita kuwatelekeza bila
kuwahudumia ingawa walistaafu wakiwa na taaluma mbalimbali hivyo
wameiomba serikali ya awamu ya tano kuwatazama kwa jicho la tatu ili
waondokane na hali ngumu ya maisha inayowakabili.
Akizungumza
mjini Morogoro kwenye kikao cha Muungano wa Wanajeshi Wastaafu Tanzania
(MUWAWATA) mwenyekiti wa muungano huo Sajent Taji mstaafu Asseidy
Mayuggi amesema Tanzania inashindwa kuendelea kiuchumi kutokana na
serikali kutumia wataalamu wa nje huku wakiwa na hazina ya wanajeshi
wastaafu wenye uwezo wa kushiriki katika kufanya kazi na kuchangia pato
la taifa.
Wamemuomba amiri jeshi mkuu Rais wa awamu ya tano Dkt John Magufuli kutumia mamlaka aliyonayo kuwatumia wastaafu hao.
Kwa
upande wao wajane wa wanajeshi waliofariki wakiwa kazini wamelalamikia
jeshi hilo kusitisha malipo ya kujikimu pamoja na kuwasomesha yatima
walioachwa na wazazi wao ambapo wamesema wameshindwa kuwaendeleza
kimasomo kutokana na hali ngumu ya maisha inayowakabili.
Katika
kuhakikisha wastaafu wanaepuka kuishi maisha ya utegemezi mfuko wa
taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) umeendelea kusajili wanajeshi wastaafu
wajiunge na mfuko huo kwa lengo la kupatiwa huduma za matibabu bure,
kupata mkopo wenye riba nafuu pamoja na mitaji itakayowawezesha
kuendesha maisha kuliko kuendelea kuilalamikia serikali.
Post a Comment