Mwanasheria
mkuu wa serikali, George Masaju amepinga hoja zilizoibuliwa na UKAWA
kuhusu uhalali wa rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Dkt Shein,
kuhudhuria kwenye uzinduzi wa Bunge.
Masaju
ametumia ibara ya 102 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania
kupangua hoja hizo ambayo inaeleza kuwa, kutakuwa na serikali ya
Zanzibar itakayo julikana kama serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambayo
itakuwa na mamlaka katika Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo mambo ya
muungano kwa mujibu wa masharti ya katiba hii.
Pia
ametumia ibara ya 103 ibara ndogo ya kwanza ya katiba ya jamhuri
inayosema kuwa, kutakuwa na kiongozi wa serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar ambae ndiye atakuwa rais wa Zanzibar na mkuu wa serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar na vilevile mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.
Baada
ya Ibara hizo, akajielekeza kwenye katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984
katika Ibara yake ya 26 ambayo inasema, kutakuwa na rais wa Zanzibar
ambae atakuwa mkuu wa nchi ya Zanzibar, kiongozi wa serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi.
Hali
kadhalika akanukuu Ibara ya 27 ambayo inaeleza namna rais wa Zanzibar
atakavyo patikana ambayo inasema kwamba, rais atachaguliwa kufuatana na
katiba hii na kwa mujibu wa sheria yoyote itakayotungwa na baraza la
wawakilishi kuhusu uchaguzi wa rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi
na uchaguzi wa rais utafanyika katika tarehe itakayowekwa na tume ya
uchaguzi (ikiwa na maana ya ZEC).
Aidha,
alinukuu Ibara ya 28 (a) ya katiba ya Zanzibar ambayo inaeleza kwamba,
kufuatana na katiba hii, mtu ataendelea kuwa rais mpaka:
a) Rais anaefata ale kiapo cha kuwa rais
Baada
ya hoja hizo akahitimisha kwa kusema, kwa kuwa tayari tume ya uchaguzi
ya Zanzibar (ZEC) imefuta uchaguzi, na kwa kuwa tayari tume hiyo
imetangaza tarehe ya kufanyika uchaguzi mkuu mwingine visiwani Zanzibar,
na kwa kuwa hakuna mtu yeyote alieapa kiapo cha urais tofauti na rais
wa sasa wa Zanzibar, Dkt Shein. Hivyo Dkt Shein anatambulika kama rais
wa Zanzibar na ana uhalali wote wa kuhudhuria katika uzinduzi wa Bunge
la 11.
Post a Comment