YAH: SHEREHE ZA KUMUAPISHA WAZIRI MKUU MTEULE
Sherehe za kumuapisha Mhe. Majaliwa
Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu Mteule zitafanyika katika Ikulu ndogo ya
Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Novemba, 2015 kuanzia saa 4.00
Asubuhi.
Sherehe hizo zinafanyika siku
moja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha jina
lake kwa kura nyingi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kufuatia uteuzi uliofanywa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mujibu wa ratiba ya sherehe
hizo, Wageni waalikwa wote wanapaswa kuwasili katika Ikulu ya Chamwino
kuanzia majira ya saa mbili asubuhi.
Sherehe hizo zinatarajiwa
kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Marais Wastaafu, Mawaziri
Wakuu wastaafu na waheshimiwa wabunge.
Imetolewa na Idara ya Habari MAELEZO
19 Novemba, 2015
Post a Comment