Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imemkuta na hatia aliyekuwa
Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Taifa (ATCL), Bw. David Mattaka na
wenzake wawili baada ya mashahidi 13 kutoa ushahidi wao mahaakamni hapo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama
hiyo, Emmilius Mchauru amesema mahakama imejiridhisha bila shaka baada
ya upande wa mashitaka kuwasilisha mashahidi 13 kuhusu tuhuma
zinazomkabili kigogo huyo wa zamani wa ATCL za matumizi mabaya ya ofisi
kwa kutanagza zabuni ya ununuzi wa magari yaliyochakaa 26 na
kuisababishia hasara serikali ya mabilioni ya shilingi.
Washitakiwa wote watatu wakiongozwa na
mawakili wao walikubali kutoa ushahidi wao kwa kula kiapo ambapo
mashahidi wa washitakiwa hao wanatarajiwa kuanza kuwatetea mapema
Desemba 10 na 11 huku dhamana zao zikiendelea.
Katika shauri hilo la matumizi mabaya
ya ofisi linawakabili David Mattaka aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, Kaimu
Ofisa Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa ATCL na Elsaph Ikomba na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Ndani, Wiliam Haji.
Post a Comment