HATIMAYE aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi
CUF aliyejiuzulu uenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba
ameibuka na kusema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.
John Magufuli anakabiliwa na hali ngumu ya bajeti kwa kipindi kijacho
cha miaka mitano.
Akizungumza na wanahabari katika ofisi za chama hicho zilizopo
Buguruni jijini Dar leo, Lipumba amesema Rais Magufuli anakabiliwa na
mambo kadhaa yakiwemo ya hali ngumu ya bajeti ya serikali kufuatia
taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwezi Oktoba 2015 kuonesha kuwa,
mwaka wa fedha 2014/2015 serikali ilipanga kukusanya mapato ya ndani ya
shilingi bilioni 12,178 ikiwa sehemu kubwa ni makusanyo ya mapato ya
Tanzania Revenue Authority (TRA).
Aidha aliendelea kufafanua kuwa, serikali ilikusanya shilingi bilioni
10,507 mapato halisi ukilinganisha na bajeti kwa kiasi cha shilingi
bilioni 1,671 sawa na 14% ya malengo ya bajeti.
Akaongeza kuwa, halmashauri za wilaya, miji na majiji zilitarajiwa
kukusanya shilingi bilioni 458.5 lakini zilifanikiwa kukusanya shilingi
bilioni 360.1 sawa na 78.5% ya malengo ya bajeti.
Alisema kwa upande wa misaada, bajeti ya shilingi bilioni 1,481
ilitolewa na upungufu ukiwa ni bilioni 457 sawa na asilimia 31 ya bajeti
huku mikopo yenye masharti nafuu ya shilingi bilioni 1,000 ikifanikiwa
kwa bilioni 859.
Kwa upande wa wanahabari waliomuuliza maswali kuhusu kurudia uchaguzi
wa urais katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Lipumba alisema, Rais
Magufuli anao uwezo wa kuishauri Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC) kutoa uamuzi wa kumtangaza mshindi wa urais na sio kurudia
uchaguzi kama ilivyoamuliwa na mwenyekiti wa Tume.
“Kila kitu kiko wazi, mawakala walipata nakala za kila jimbo kwa majimbo yote 54, binafsi namuomba aishauri Zec itangaze matokeo halisi tofauti na kurudia uchaguzi,” alisema Lipumba.
“Kila kitu kiko wazi, mawakala walipata nakala za kila jimbo kwa majimbo yote 54, binafsi namuomba aishauri Zec itangaze matokeo halisi tofauti na kurudia uchaguzi,” alisema Lipumba.
Akizungumzia kasi ya Rais Magufuli, Pro.Lipumba alisema anaiunga
mkono hasa kupitia kauli mbiu yake ya ‘Hapa Kazi Tu’ huku akisisitiza
kauli hiyo kuendelea kuzaa matunda.
Akampongeza kwa ziara zake za kushitukiza akieleza kuwa zinazaa
matunda huku akionesha mfano mzuri pale alipotembelea Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili na kujionea hali halisi ya mashine za CT Scan na MRI
zikiwa mbovu na baada ya siku chache kuwa zimetengenezwa.
Hata hivyo alisisitiza kuwa ziara hizo hazitakuwa na tija kama bajeti
ya maendeleo haitakidhi matatizo ya Watanzania kama vile afya bora,
elimu, ajira, kupambana na rushwa, miundo mbinu na kilimo bora.
(Stori na Denis Mtima/GPL)
Post a Comment