Pamoja na
wenyewe kudai hawajui kilichotokea, mastaa wawili wenye sura za mauzo
kunako sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Wema Isaac Sepetu,
kwa sasa wanadaiwa kufikia pabaya kufuatia bifu zito linalofukuta kati
yao.
Habari za mjini zinadai kwamba, Wema
amekuwa akishtushwa na kuchukizwa na kitendo cha Lulu kuwa upande wa
aliyewahi kuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kiasi cha
kwenda nyumbani kwake, Madale-Tegeta jijini Dar, usiku wa manane na
kujiachia na jamaa huyo anavyotaka.
“Kama mtakumbuka, kabla ya kifo cha
Kanumba (Steven), Wema na Lulu walikuwa ni mashosti kama ilivyokuwa kwa
Wema na Snura (Mushi) au Wema na Kajala (Masanja) au Wema na Aunt
(Ezekiel).
“Lakini baada ya jamaa (Kanumba)
kuondoka na kisa kizima cha Lulu ndipo Wema akavunja urafiki na Lulu kwa
sababu Kanumba aliwahi kuwa ‘mtu’ wa Wema kama ilivyo kwa Diamond.
“Ulipita ukimya wa muda mrefu bila Wema na Lulu kuwa mashosti zaidi ya salamu.
“Lakini mambo yalianza tena kuwa mabaya
baada ya Lulu kumponda Wema alipokuwa akigombea Ubunge wa Viti Maalum
kupitia CCM (Chama Cha Mapinduzi).
“Sasa hivi ishu ni kitendo cha Lulu
kujiachia na Diamond kwenye birthday ya Rome Jones (binamu na DJ wa
Diamond) kisha ile pati ya birthday Diamond kuifanyia nyumbani kwake
huku (Lulu) akitupia picha za mafumbo yaliyoelekezwa kwa Wema.
“Hicho ndicho kinachoendelea na unaambiwa hali ni tete mno,” kilisema chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao.
Baada ya kupata ‘ubuyu’ kamili, Amani lilimtafuta Wema na kummwagia data ambapo alionesha kushtushwa na kudai kwamba hata yeye anashangaa ni nini kimetokea.
Kwa upande wake Lulu hakupatikana hewani
lakini kwa mujibu wa mahojiano aliyofanya hivi karibuni juu ya uhusiano
wake na Wema, mwanadada huyo alikiri kuwa rafiki wa Wema kitambo hicho
lakini akasema hajui ni nini kilichotokea zaidi ya kwamba huwa
wanasalimiana tu wanapokutana.
Kabla ya mambo kwenda mrama, Lulu na
Wema walikuwa mashosti wakubwa ambapo gazeti hili liliwahi kuwashuhudia
wakiwa lokeshi na kulala pamoja chumba kimoja kama mtu na dada au mtu na
mdogo wake.
Post a Comment