Msanii
mwanadada Shilole ambae kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa
'Nyang'anyang'a' amefunguka na kuwataka watu ambao wanamkejeli kuwa ana
miguu mibaya wamuache na miguu yake hiyo.
Shilole
jana alipost picha kwenye Instagram ambayo ilikuwa ikionyesha sehemu
kubwa ya miguu yake na baadhi ya watu walianza kusema kuwa afunike miguu
yake hiyo kwani ni mibaya wengine walionyesha kupenda picha ile huku
wengine wakimpa sifa kuwa ni mrembo, lakini hizo comment chache
zilionyesha kumkera Shilole kiasi cha kuamua kufunguka kwa wale ambao
wana kazi ya kuwakosoa watu.
“Nyie
wenye kazi ya kukosoa wenzenu, OOoh miguu mibaya mara ipo kama fito
sijui nini. Niacheni na fito zangu mwenywe nimeridhika sasa kama mnataka
kushindana na Mungu jiumbeni nyinyi na mapungufu yenu mliyonayo na
siachi kuzianika fito zangu mbona mtakereka sanaaa,” aliandika Shilole.
Katika
hatua nyingine baadhi ya mashabiki wa Shilole walionyesha kutopendezwa
na baadhi ya tabia ya watanzania kuanza kukosoana na kusemana vibaya
kama ambavyo wamefunguka hapo chini.
Rebecca2559: “Jaman watanzania tupunguze majungu mtu anaishi atakavyo mwacheni Shilole afanye atakacho kila mtu na maisha yake”.
Sabrasuy8:
Kama wao wana miguu mizuri basi kuna walichokosa. Achana nao hawaigi
kua kama wewe bali wanafikiri kuponda ndio uhodari wao, achana nao
wanakukubali ila kukupongeza wanaona haya hao.
Post a Comment