Wazanzibari wanaoishi nchini Uingereza jana walifanya
maandamano wakidai haki ya kutangazwa ushindi wa Chama Cha Wananchi
(CUF) katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Octoba 25 mwaka huu
Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Zanzibar Welfare Association (ZAWA) ambapo wazanzibari hao walitoka
maeneo mbali mbali katika miji yao na kukusanyika katika eneon la
Downing Street kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron
na uongozi huo kukabidhi barua yao yenye malalamiko kutaka suala la
Zanzibar lishughulikiwe.
Maandamano hayo yalifanyika
kwa lengo la kuongeza shindikizo kwa mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kuchukua hatua za haraka ya kuhakikisha Tume ya Uchaguzi
Zanzibar (ZEC) inakamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Zanzibar iliingia katika mkwamo wa kisiasa baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha Octoba 28 kutangaza kuufuta uchaguzi wote kwa madai kwamba ulikumbwa na matatizo mbali mbali.
Wakati
jecha akitoa tangazo la kufuta matokeo bila ya kushauriana na tume yake
alikuwa tayari ameshatangaza matokeo ya kura za urais za majimbo 31
kati ya 54 ya Zanzibar pia washindi wa nafasi za uwakilishi na udiwani
katika majimbo hayo walishatangazwa na walishakabidhiwa vyeti vyao.
Rashid
Ali ambaye ni kiongozi wa ZAWA alisema jana kuwa wamewasilishwa barua
hiyo wakiamini kwamba suala la Zanzibar litashughulikiwa ili wananchi wa
Zanzibar waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Mwakilishi
wa ZAWA, Hassan Khamis alisema wameamua kupeleka barua kwenye ofisi za
waziri Mkuu wakiamini suala hilo litashughulikiwa ikiwa ni pamoja na
serikali ya Tanzania kuchukua hatua madhubuti na za haraka kaika
kushughulikia suala hilo ambalo limewaweka wazanzibari roho juu.
Post a Comment