Watu
watatu raia wa china wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani Mbeya kwa
tuhuma za kukamatwa na pembe 11 za faru wakijaribu kuziingiza nchini
wakitokea nchi jirani ya Malawi.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mbeya, kamishana msaidizi mwandamizi wa Polisi,Ahamed
Msangi amesema watuhumiwa hao ambao wote ni raia wa china,wamekatwa
katika mpaka wa Tanzania na Malawi wa Kasumulu wilayani Kyela wakati
wakijaribu kungia nchini kwa gari aina ya TOYOTA HILUX.
Aidha
Kamada Msangi amesema kuwa gari hilo baada ya kukaguliwa ndipo
likagundulika kubeba nyara za serikali ambazo ni pembe 11 za faru
walizozificha chini ya CHASES ya gari hilo.
Maofisa
wa idara za uhamiaji na mamlaka ya mapato Tanzania TRA, ambao pia
wameshiriki katika zoezi la kuwatia mbaroni wachina hao, wamesema kuwa
licha ya wachina hao kuwa na Pasport zinazowaruhusu kuingia nchini
kihalali,lakini ni kosa kuingia na vitu ambavyo vimezuiwa,hivyo kwa
kufanya kosa hilo wanaweza kuchukuliwa hatua za Kisheria.
Post a Comment