Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UKAWA YASALIMU AMRI KWA SERIKALI

* YAFUTA MKUTANO WAKE BAADA YA AGIZO ZITO NA KALI 

* YATOA TAARIFA RASMI, HII HAPA ....


Taarifa inatolewa kwa wapenzi, mashabiki, wafuasi na wanachama wa CHADEMA, wana UKAWA na umma wa Watanzania wote wapenda mabadiliko kwa ujumla kuhusu mkutano mkubwa wa hadhara wa kesho katika Viwanja vya Jangwani, jijini Dar Es Salaam ambao umeshatangazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari, umeahirishwa hadi hapo maelekezo na utaratibu mwingine utakapotolewa baadae.

Ni vyema kuwataarifu ujumbe huu mapema maelfu ya Watanzania ambao tunajua wamejiandaa kuhudhuria kwa wingi kusikia 'neno kutoka kwa Rais wa Mioyo ya Watanzania' na viongozi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA juu ya uelekeo wa nchi kwenye mkutano huo ambao pia ulilenga kuwatambulisha wabunge wote wa UKAWA na kuwashukuru Watanzania kwa namna walivyounga mkono agenda za MABADILIKO kwenye mapambano makubwa ya ushindi wakiwa begabega na Jemadari Lowassa, Babu Duni, wagombea ubunge na udiwani wa UKAWA.

Makene

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top