Watu
wanne akiwemo askari Polisi, mkaguzi na wasimamizi wa mitihani ya
kidato cha nne Arusha wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kukutwa
wakivujisha mtihani wa Kiswahili uliokuwa unatarajiwa kufanyika Novemba
20 mwaka huu.
Mtihani
huo ulijulikana kuwa umesambaa katika shule ya Sekondari Arusha baada
ya wanafunzi kugawiwa na wakati wanausoma ndipo walipogundua kuwa si wa
Novemba 2 kama ulivyopangwa bali ni wa Novemba 20 ndipo walipoamua kutoa
taarifa wasimamizi.
Mkurugenzi
wa jiji la Arusha Idi Juma alisema mtihani huo ni wa watahiniwa wa
kujitegemea ambao hufanya mitihani miwili na watu hao walijichangaya
badala ya kuchukua mtihani wa Kiswahili wa awamu ya kwanza walichukua wa
awamu ya pili.
Hata
hivyo Mkurugenzi huyo hakuweza kuwataja majina wahusika kwa madai kuwa
bado wanaendelea na upelelezi kubaini chanzo cha tukio hilo.
Post a Comment