JUKWAA la Katiba Tanzania (Jukata) limeitaka Serikali ya Awamu ya Tano kuanza kazi ya kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya.
Ni
kutokana na serikali ya Rais Jakaya Kikwete iliyokoma Mei 5 mwaka huu
baada ya Dk. Magufuli kuapishwa, kura ya maoni ilipangwa kufanyika
Aprili 30 mwaka huu lakini haikufanyika.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Jukwaa
la Katiba, Deus Kibamba amesema kuwa, kushindwa kupatikana kwa Katiba
ndani ya muda kulizua hofu kwamba mchakato huo ungeweza kukwama.
“Kama
Jukwaa tumeendelea kufuatilia kwa ukaribu, kutafiti na kushauriana juu
ya mchakato ulipofikia na namna ya kutoka hapo kama taifa katika kipindi
chote tangu mchakato uliposimama,” amesema Kibamba.
Kibamba
amesema kwamba, baada ya kushindikana kwa jaribio la kuunganisha kura
ya maoni na uchaguzi mkuu, kuna taarifa kuwa Tume ya Uchaguzi ya Taifa
(NEC) kwa sasa inaanza maandalizi ya kuitisha upya kura ya maoni ili
Watanzania waweze kuipigia kura ya ndiyo au hapana.
Aidha,
mchakato wa Katiba Mpya ulianza mwaka 2011 ambapo ulitarajia kukamilika
kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu ambapo serikali ilitaja kuwa Aprili
26 2014 kama siku ambayo katiba mpya ingepatikana.
Amesema,
hata baada ya kushindikana, lengo la serikali lilibaki kuwa kura ya
maoni juu ya katiba iliyopendelezwa ifanyike Aprili 30 mwaka huu. Hata
hivyo, tarehe hiyo ilipita bila kura ya maoni kufanyika.
“Kwa
tathimini ya JUKATA , mchakato wa katiba ulianza vizuri hadi kufikia
rasimu ya pili ya katiba (Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba )
lakini kutekwa kwa mchakato wa katiba wakati wa bunge maalum ilikuwa
mwanzo wa kufifia kwa hamasa ya mchakato wa katiba,” amesema Kibamba.
Hata
hivyo, kwa kuwa mchakato wa kuandika katiba mpya ulianzishwa na Rais wa
Awamu ya Nne, Kikwete na haukukamilika, hivyo JUKATA limemtaka Rais
Magufuli baada ya kuunda Baraza la Mawaziri.
Mbali
na hilo, JUKATA limesema kuwa limesikitishwa na kitendo cha Jeshi la
Polisi kuvamiwa na kuwakamata waangalizi wa uchaguzi wa mwamvuli wa
Asasi za Kiraia zinazoangalia uchaguzi ukijulikana kama TACCEO ambao
walikamatwa Oktoba 29 mwaka huu.
Pia
JUKATA limelaani vikali mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa
wa Geita, Alphonce Mawazo ambaye pia alikuwa mgombea wa ubunge katika
uchaguzi uliopita.
Post a Comment