Na Nathaniel Limu
[SINGIDA] Jeshi
la Polisi Mkoani Singida, limefanikiwa kumuawa Dotto William
anayekadiriwa kuwa na umri kati ya 30 na 33 mkazi wa Kibaoni kata ya
Kindai tarafa ya Unyaminkumbi mjini Singida anayesadikika kuwa ni
jambazi sugu,wakati wa kupukushani za kumnyang’anya askari silaha.
Mtuhumiwa
huyo ujambazi na kinara wa matukio ya utekaji magari kwenye eneo la
barabara kuu ya Singida-Nzega, alipigwa risasi wakati alipojaribu
kupambana na askari ana kwa ana.
Marehemu
huyo, anadaiwa kutoka gerezani hivi karibuni, kutokana na msamaha rais,
serikali ya awamu ya nne, chini ya Dk. Jakaya Kikwete
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,ACP Thobias Sedoyeka,alisema tukio
hilo limetokea novemba 19 mwaka huu saa 5.30 asubuhi huko katika maeneo
ya Kindai mjini hapa akiwa amejificha kwenye nyumba ya mtu mmoja ambaye
bado anatafutwa na polisi.
Alisema
kuwa, tukio hilo lilitokea katika pori la kijiji cha Minyughe, wilayani
Ikungi, wakati mtuhumiwa huyo alipoongozana na askari polisi kwenda
kuwaonyesha silaha aliyoificha, anayoitumia kuteka magari.
Alisema
kuwa, licha ya marehemu kuhusishwa na matukio mengi ya uhalifu, ikiwemo
utekaji wa kituo cha mafuta Igunga, mkoani Tabora na magari katika
mlima Kititimo, mjini Singida, siku ya novemba 18 saa 4:00 usiku mwaka
huu, aliteka pia magari matano, wilayani Mkalama.
Kamanda
Sedoyeka alisema kuwa siku hiyo mtuhumiwa huyo akitumia pikipiki yenye
namba za usajili MC 855 AWF Sunlag na wenzake kadhaa,alifanya uhalifu
katika kijiji cha Milade wilaya Mkalama kwa kupora abiria fedha na vitu
mbalimbali, kabla ya kutokomea kusikojulikana.
Ilidaiwa
kabla ya uhalifu huo, alitega mawe makubwa barabarani, hali
iliyomrahisishia ujambazi wake, ikiwmo kuwapiga kwa fimbo, marungu na
kuwatishia abiria kwa kutumia bunduki aliyokuwa nayo.
Alisema
kuwa, baadaye polisi walifanikiwa kumkamata jambazi huyo akiwa na
Pikipiki yake ndani ya nyumba moja iliyopo mtaa wa Kibaoni, Singida
mjini, na baada ya mahojiano alikiri na kwenda kuwaonyesha bunduki
anayotumia kwenye ujambazi, ikiwemo utekaji magari.
Sedoyeka
alisema baada ya kufika eneo alikoficha silaha hiyo katika pori la
Minyughe, wilaya ya Ikungi, lilifanikiwa kutoa bunduki hiyo aina ya SAR
namba 51025, ikiwa imefichwa kwenye kichaka, ikiwa na risasi zake tatu.
Hata
hivyo Sedoyeka alisema kuwa, askari aliyeongozana naye alipotaka
kuichukua, jambazi hilo lilimrukia kwa lengo la kumdhuru, lakini askari
mwingine alifanikiwa kumpiga risasi na hatimaye kupoteza maisha wakati
likipelekwa kutibiwa katika hospitali ya Mkoa.
Post a Comment