Kassim Majaliwa ambaye ni mbunge wa Ruangwa sio jina geni katika medani za soka, kama unakumbuka vizuri Kassim Majaliwa aliwahi kuwa kocha wa mpira wa miguu na aliwahi kuifundisha klabu ya Singida United, kazi ya ukocha kwa waziri mkuu huyo haikuwa ya kubahatisha bali alikuwa akitambulika rasmi kama kocha mwenye leseni daraja B na shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF).
Afisa habari wa Azam FC Jafari Iddi Maganga amezungumzia na kumpongeza MhKassim Majaliwa
“Uongozi
wa Azam FC na bodi ya uongozi ya Azam FC inampogeza Kassim Majaliwa kwa
kuteuliwa kuwa waziri mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
lakini kwa wale ambao hawafahamu Mh Majaliwa aliwahi kuwa kocha wa klabu
ya Singida United miaka ya nyuma ana leseni B ya ukocha kutoka kwa
shirikisho la soka barani Afrika CAF hivyo tumefuraishwa kwa yeye
kushika nafasi hiyo” >>> Jafari Iddi
Msikilize hapa Jafari Iddi akimzungumzia Mh waziri Mkuu Majaliwa
Post a Comment