MSANII
mtajika Rehema Chalamila, almaarufu Ray C ameomba radhi kwa mashabiki
na wafuasi wake kufuatia video iliyomwonyesha akicheza densi akiwa uchi
wa mnyama kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.
Akiongea kwenye redio ya Clouds FM ya Tanzania, Ray C alikubali kuwa aliyekuwa akicheza densi akiwa uchi ni yeye lakini hakujua aliyeiposti kwa akaunti yake.
“Ni kweli kwamba video iliwekwa kwa akaunti yangu ya Instagram ila mimi mwenyewe sikuiweka,” alisema mkali huyo wa kibao Wanitafutia Nini.
Ray
C alifichua kuwa video hiyo ilirekodiwa kwa matumizi ya kibinafsi ya
mchumba wake. Pia alisema kuwa simu yake iliibwa na mtu ambaye anaamini
ni mmoja kati ya marafiki zake na anakisia rafiki huyo ndiye aliiposti
kwenye mtandao.
“Simu
yangu ilipotea Jumatatu. Nina uhakika kuwa ni rafiki yangu ninayemjua
vizuri aliweka video hiyo baada ya kuitoa kwa simu yangu.
Kwa
kawaida akaunti yangu ya Instagram huwa wazi kwa sababu simu ni kifaa
changu binafsi. Sijawahi kufikiria kwamba mtu yeyote anaweza kuniibia
simu,” akaeleza Ray C.
Msanii huyo hakusita kusema kuwa mchumbva wake ndiye aliirekodi video hiyo kwa matumizi yao binafsi.
“Nimeripoti kwa kampuni ya huduma za simu Vodacom na wakazuia laini yangu.Vodacom imefuta video hiyo kutoka kwa akaunti yangu,” akaongeza.
Ray C aliomba msamaha kutoka kwa wafuasi wake na umma kwa jumla.
“Sina
la kusema. Naomba radhi kwa mashabiki wangu na umma. Naomba wanielewe
kama nilivyoeleza kisa hiki. Nimepiga ripoti kwa polisi.,” Ray C
akasema.
Post a Comment