Meza Kuu , Kutoka Kushoto ni Ndugu Maumba Mgaya, Mwenyekiti wa Jumuiya, Bi Magreth Mjindo na Ndugu Andrew Katibu.
Mnano
tarehe 7/11/2015, Jumuiya ya watanzania waishio nchini Thailand
ilikutana na kujadiliana mambo mbalimbali ya jinsi gani wanaweza
kusaidiana katika mambo mbalimbali, TIT ilianzishwa mnano mwezi wa nne
mwaka, 2015 na inahusisha watanzania mbalimbali,
wanafunzi,wafanyabishara na wafanyakazi waishio na kufanya nchini
Thailand. Mkutano mkuu wa Jumuiya ulifanyika katika Hoteli ya Amari
Boulevard Mjini Bangkok na kuhudhuriwa na wanajumiya mbalimbali.
Pamoja
na kujadiliana mambo mbalimbali kulifanyika uchaguzi wa viongozi ambapo
wafuatao walichaguliwa kuwa viongozi wa jumuiya kwa kipindi cha
mwaka mmoja:
Mwenyekiti: Bwana Maumba Mgaya
M/Kiti: Bw. Alois Ngonyani
Katibu: Bw.Andrew Wajama
Katibu Msaidizi: Bw. Emmanuel Mushi
Mhazini: Bw. Adolf Kigombola
Mhazini Msaidizi: Bi.Tumaini Kalindile
Afisa Mawasiliano: Bw. Emmanuel Nyamageni
Afisa Mawasiliano Msaidizi: Bw. Jordan Hossea.
Pamoja
na uchaguzi kulifanyika sherehe fupi ya kumpongeza Bi Magreth Dionis
Mjindo ambaye amemaliza Shahada ya uzamili ya maendeleo ya jamii na
anarejea nyumbani kulitumikia Taifa.
Jumuiya
inapenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wao Ndugu Florean
Rwehumbiza, Dada Lucy Kileo pamoja na Ndugu Kivea Mbwana (Homeboy) kwa
kusimamia uchaguzi na kufanikisha kufanyika kwa mkutano huu muhimu.
Shukrani za pekee ziende kwa Kampuni ya Broadhurst Pacific, kwa
kusimamia, kudhamini na kufanikisha tukio hili muhimu.
Mhazini wa Jumuiya Ndugu Adolph Kigombola akisoma taarifa ya fedha.
Tunapenda
kuwapongeza na kuwashukuru viongozi waasisi wa jumuiya waliomaliza muda
wao ambao ni ndugu Saidi Husein Kitenge Mwenyekiti wa kwanza wa jumuiya
na makamu wake Ndugu Masui Vicent Munda na ndugu Antidius Muchunguzi
bila kuwasahau maafisa mawasiliano wetu akiwemo ndugu Felix Mwema na Bi
Diana Richard.Mungu awabariki kwa kuitumikia vema TIT.
Aidha
Jumuiya inawakaribisha watanzania mbalimbali walioko nchini Thailand au
wanaotarajia kuja nchini Thailand kushirikiana na jumuiya yetu.
Umoja ni nguvu
Imetolewa na Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Thailand (TIT)
+66947230002/+66972494819
Mkutano Mkuu ukiendelea.
Baadhi ya Watanzania Waishio nchini Thailand.
Mkutanoni.
Timu ya Wadhamini wakisimamia Uchaguzi.
Bw. Florean Akikabidhiwa keki ya kuzaliwa na Bi Lucy.
Ndugu Florean akimkabidhi Bi Magreth Zawadi kwa niaba ya Jumuiya.
Wanajumuiya Wakipata Chakula cha Pamoja.
Watanzania Waishio Thailand wakipata chakula cha pamoja.
Watanzania Waishio Thailand Wakiwa Katika Picha ya Pamoja.
Post a Comment