Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen KijoBisimba anatarajia
kusafirishwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.
Novemba 7, mwaka huu Dk Bisimba alipata ajali ya gari katika
barabara ya Ali Hassan Mwinyi na kuvunjika mshipa wa paja na
goti sanjari na kujeruhiwa kichwa,bega na mgongo.
Akizungumza
jana akiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI)
ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam, Dk
Bisimba alisema kwa sasa anaendelea vizuri na kwamba anatarajiwa
kupelekwa nchini humo na
watoto wake kwa matibabu zaidi.
Alisema safari yake hiyo siyo kwa sababu ya upungufu wa huduma aliyoipata kutoka MOI bali ni
kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi wa mwili wake.
“Namshukuru Mungu naendelea vizuri. Tangu nimekuja hapa MOI, nimesikilizwa na
kuhudumiwa vizuri. Watoto wangu wanashugulikia usafiri na siku yoyote naenda India ,”alisema.
Meneja Uhusiano MOI, Jumaa Almasi alisema kuwa Dk Bisimba bado anahitaji uangalizi wa hali
ya juu katika kipindi hiki kutokana na kupata majeraha mengi kwenye mwili wake. “Hali ya Dk
Bisimba imevunja rekodi.
Mbali na kumshughulikia sehemu hizo mbili (paja na goti), kutokana na
kuwa na kisukari na presha tumeshindwa kulazimisha matibabu ya haraka kwa viungo vyote,”
alisema.
Post a Comment