CHAMA
cha Walimu Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam, kimesema Serikali imeanza
kulipa deni la madai ya walimu kiasi cha Sh 1,936,572,146.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa CWT wa mkoa huo, Amina
Kisenge, alisema kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi Julai 2015
walikuwa wanaidai Serikali kiasi cha Sh 3,916,432,471.
Alisema kwa sasa deni lililobaki ni Sh 1,979,860,325 ambazo bado walimu wanadai.
Alisema
pamoja na changamoto hiyo nyingine ni mfuko wa PSPF kutowalipa walimu
wastaafu kwa wakati na kudai kuwa walimu waliostaafu kuanzia Januari
hadi Septemba 2015 hawajalipwa mafao yao.
“Kutokana
na hali hiyo, tunatoa rai kwa Rais John Magufuli amalize usumbufu huu
kwa watumishi waliotumikia Taifa kwa uadilifu ili waweze kulipwa mafao
yao,” alisema.
Alisema
kilio chao kikubwa kwa Rais Magufuli ni Serikali kupitia Mdhibiti wa
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kuanzisha kanuni mpya (kikokotoo)
cha 1/580 inayoonyesha mafao ya walimu yanayolipwa kwa mkupuo toka
kanuni ya awali yaani 1/540.
Kisenge
alisema jambo hilo halikubaliki, hata kama walimu walioko kazini sasa
hawahusiki na kanuni hii kwasababu inaanza kutumika kwa wale
walioajiriwa kuanzia Julai mosi mwaka 2014.
“Kwa
sababu hii hatukubaliani na msimamo wa SSRA na tunayapinga mabadiliko
haya kwa nguvu zote kwani watakaoathirika na kanuni hiyo ni walimu
ambao ni watoto wetu.
“Eneo
lingine ambalo ni kero kwetu ni walimu Mkoa wa Dar es Salaam
kutopandishwa madaraja kwa wakati, pia wanaostahili kupandishwa madaraja
kwa mwaka husika sio wote wanaopandishwa na wanaopandishwa
hawarekebishiwi mishahara yao,” alisema Kisenge.
Aliitaja
kero nyingine kuwa ni Wakurugenzi wa Manispaa kutotekeleza maagizo ya
kupanua wigo wa madaraja ya walimu kama yalivyoainishwa kwenye
waraka wenye kumbukumbu namba CAC 2015/22801/D ya Julai, 2014.
Post a Comment