Vyama vya upinzania kisiwani Zanzibar vimetofautiana kuhusu uamuzi wa mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa maelezo kuwa haukuwa huru na haki.
Jana Chama Cha ACT-Wazalendo kiliunga mkono chama cha CUF, kupinga uamuzi huo wa Mwenyekiti wa ZEC.
Akiongea
na waandishi wa habari visiwani humo, Makamu mwenyekiti wa
ACT-Wazalendo, Ramadhani Suleiman alisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru
na haki kama ulivyoshuhudiwa na waangalizi wote wa ndani na nje ya nchi
na kuitaka Tume hiyo kuendelea na zoezi la kuhakiki matokeo na
kumtangaza mshindi.
Wakati
huohuo, vyama vya CCK, TLP na SAU wao kwa pamoja walijitokeza na kuunga
mkono uamuzi uliofanywa na mwenyekiti huyo wa ZEC wakidai kuwa uchaguzi
huo ulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu na kasoro nyingi
zilibainika hasa katika visiwa vya Pemba.
“Tunaunga
mkono kauli iliyotolewa na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
Zanzibar, ya kufuta matokeo ya uchaguzi huo kutokana na vikwazo ambavyo
Tume hiyo ilikabiliana navyo katika uendesha uchaguzi huo,” alisema mmoja kati ya wawakilishi wa vyama hivyo.
Mwenyekiti
wa ZEC alitangaza kufuta matokeo ya uchaguzi huo muda mfupi baada ya
mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kutangaza kuwa amekusanya
matokeo ya vituo vyote na kubaini kuwa yeye ndiye mshindi huku akiitaka
Tume hiyo kumtangaza.
Uchaguzi
huo ulishuhudiwa kuwa na wagombea wa urais 14 lakini wagombea wawili,
Maalim Seif Sharif Hamad (CUF) na Rais wa sasa, Dkt. Ali Shein (CCM)
ndio waliokuwa na ushindani mkubwa zaidi.
Post a Comment