Walinzi
wawili wanaolinda katika baa ya Wacha Waseme na Lunguya mjini Geita
wamejeruhiwa na vitu vyenye ncha kali ambavyo vimesababisha kifo cha
mlinzi mmojawapo.
Mlinzi huyo aliyejulikana kwa jina moja la Michael amefariki dunia baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita.
Tukio
hilo limejiri majira ya usiku wakati walinzi hao wakiwa wamelala katika
lindo ambapo watu wasiojulikana wanadaiwa kuvamia na kuwashambulia na
kuvinjwa katika baa ya lunguye na kuiba shilingi elfu tisini na nane.
Majeruhi ambao walifikishwa katika Hospitali ya Geita majira ya asubui na kupewa matibabu ambapo mchana Michael alifariki dunia.
Wananchi
wa Geita wamesema kuwa hili ni zaidi ya tukio la tano linalohusu
walinzi kuuwawa na kuomba jeshi la Polisi kuhakikisha wanawakamata
watuhumiwa waliohusika.
Kaimu
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Peter Kakamba amethibitisha
kutokea kwa Tukio hilo na msako unaendeshwa wa kuwakamata waliohusika.
Majeruhi mmoja aliyejulikana kwa jina la Musa Buberwa bado anaendelea na matibabu Hospitalini hapa.
Post a Comment