JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 12.11.2015.
• MTU MMOJA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI JIJINI MBEYA.
• MTOTO WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA CHA MAJI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE
MMOJA MKAZI WA HORONGO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA LUCY YESAYA [22] ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUPIGWA KITU KIZITO KICHWANI NA
USONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.
MWILI
WA MAREHEMU ULIKUTWA MNAMO TAREHE 11.11.2015 MAJIRA YA SAA 06:30 ASUBUHI
HUKO KIJIJI CHA IZUMBWE SOKONI, KATA YA SONGWE, TARAFA YA USONGWE,
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI, MKOA WA MBEYA.
CHANZO
CHA KIFO CHAKE NI BAADA YA KUPIGWA KITU KIZITO SEHEMU ZA KICHWANI NA
USONI. KIINI CHA TUKIO HILO BADO KINACHUNGUZWA. UPELELEZI UNAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA
KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MPANDA
BAISKELI MMOJA AMBAYE HAKUWEZA KUFAHAMIKA JINA LAKE, JINSI YA KIUME,
UMRI KATI YA MIAKA 25 – 28 ALIFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA
NA GARI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.838 AAC AINA YA TOYOTA HIACE ILIYOKUWA
IKIENDESHWA NA DEREVA AITWAYE DEO MBILINYI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.11.2015 MAJIRA YA SAA 16:40 JIONI HUKO
ENEO LA UYOLE, KATA YA IGAWILO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA
TUKIO HILO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO
IKIWA NI PAMOJA NA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MTOTO
MWENYE UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA
PROMIS DANK MKAZI WA BWAWANI WILAYA YA CHUNYA ALIFARIKI DUNIA NJIANI
AKIWA ANAPELEKWA HOSPITALI BAADA YA KUTUMBUKIA KISIMANI.
TUKIO
HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 11.11.2015 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO
KITONGOJI CHA RAILWAY, MTAA NA KATA YA BWAWANI, TARAFA YA KIWANJA,
WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA
KUWA, MTOTO HUYO BAADA YA KUTUMBUKIA KWENYE KISIMA HICHO AMBACHO
KILIKUWA WAZI, ALIOKOLEWA AKIWA HAI LAKINI ALIFARIKI DUNIA AKIWA NJIANI
KUELEKEA HOSPITALI TEULE YA MWAMBANI KWA MATIBABU.
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI HASA KWA KUWEKA
UANGALIZI WA KUTOSHA KWA WATOTO WADOGO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA
KUEPUKIKA.
AIDHA
ANATOA WITO KWA JAMII KUFUNIKA VISIMA VILIVYOWAZI, KUFUKIA MASHIMO
YENYE MAJI KWANI NI HATARI KWA WATOTO WADOGO HASA KATIKA MSIMU HUU WA
MVUA ZA VULI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment