DAR ES SALAAM
18/11/2015
Mabadiliko ya Tabia
Nchi, uharibifu wa vyanzo vya maji katika mito mbalimbali na uchepushaji wa
maji kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji ni chanzo cha kukauka kwa
mabwawa ya maji yanayotumika katika kuzalisha umeme.
Hayo yamesemwa jijini
Dar es salaam na msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud
alipokuwa akizungumzia ukaguzi wa wezi wa umeme nchini.
“Umeme unaotumika kwa
sasa unazalishwa kwa kiasi kikubwa na gesi asilia pamoja na mafuta mazito na
diseli ambapo umeme unaotokana na nguvu ya maji unazalishwa kwa kiasi kidogo”
alisema Bi Badra.
Akizungumzia hali ya
umeme nchini, Badra alisema kwamba kwa sasa hakuna mgawo wowote unaoendelea
kwani uzalishaji ni mzuri, kiasi cha umeme kinachopatikana sasa ni megawati 1500
wakati matumizi kwa siku ni megawati kati ya 800 na 900.
Aidha Bi. Badra alisema
kwamba Wizara ya Nishati na Madini inatarajia kuunda kikosi maalumu kitakachojumuisha
wataalamu kutoka katika taasisi mbalimbali kukabiliana na wizi wa umeme nchini.
“Wizi wa umeme nchini
ni jambo linalolikosesha mapato shirika la Tanesco, hivyo kikosi hicho
kitajumuisha wataalamu kutoka TANESCO, Wizara ya Nishati na Madini pamoja na
vyombo vya usalama” alifafanua Bi Badra.
Pia Wizara
imewataharisha baadhi ya watu wanaohujumu miundombinu ya TANESCO kama kuchoma
nguzo za umeme, kuiba mafuta ya transforma pamoja na nyaya za umeme na watakaogundulika
watachukuliwa hatua za kisheria,
Hata hivyo Shirika la
umeme Tanzania TANESCO limeagizwa kuimarisha kikosi chake cha ukaguzi wa
watumiaji wa umeme ili kubaini wateja wasio waaminifu wanaoiba umeme wa
majumbani na viwandani na kuwachukulia hatua za kisheria.
Katika kuhimiza
matumizi bora ya umeme Wizara ya Nishati na Madini imezitaka taasisi mbalimbali
za serikali na zisizo za kiserikali kuzingatia matumizi mazuri ya Nishati hiyo
ili kudhibiti upotevu wa umeme.
Post a Comment