CHEZEA kifo
wewe! Mwalimu wa Shule ya Msingi Mwere ya mjini hapa ambaye jina
halikupatikana mara moja, akiwa mjamzito, amenusurika kifo baada ya
daladala walilopanda kutumbukia mtaroni na yeye kuchomokea kwenye
dirishani.
Gari likiwa limepinduka baada ya ajali hiyo.
Tukio
hilo lilijiri jirani kabisa na eneo la Kanisa la KKKT ambapo mashuhuda
walidai kwamba tukio hilo lilitokea baada ya dereva wa daladala
aliyefahamika kwa jina moja la Mathias kumuachia ‘deiwaka’ kijana
mwingine aliyetajwa kwa jina la Arird Tito.…
....Mmoja wa shuhuda akielezea jinsi ajali hiyo ilivyotokea.
Baada
ya dereva wa gari kubwa kuona hivyo hakumpa nafasi dereva huyo ndipo
akajikuta anatumbukia mtaroni.“Baada ya gari kutumbukia mtaroni, ticha
huyo na madenti wake walilazimika kuokoa maisha yao kwa kutokea kwenye
madirisha ya daladala hiyo,’’ alisema Tito ambaye alikuwa ni kondakta wa
daladala hiyo.
Hata hivyo, abiria hao hawakuumia sana zaidi ya kupata michubuko ya hapa na pale, kabla ya kupelekwa hospitalini kwa matibabu.
chanzo na global publishers.
Post a Comment