Mbunge mteule wa jimbo la Hai na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Freeman Mbowe (Chadema) amesema mchakato wa kumpata spika wa Bunge unaendelea ndani ya umoja huo.
Mbali na hilo amesema siyo dhambi kumpata spika ambaye hatokani na wabunge na asiye kuwa na chama chochote cha siasa.
Mbowe
alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu
ya mchakato wa kumpata Spika wa Bunge la kumi na Moja.
Mbowe alisema mchakato wa uspika ndani ya umoja wao unaendelea na watakapo maliza wataweka adharani majina ya watu waliochomoza.
Akizungumzia
hoja ya Spika kuwa mbunge au la alisema inafaa zaidi Spika kutokuwa
mbunge na asiye kuwa na chama chochote cha siasa.
Amesema kuwa mbunge siyo sifa ya kuwa unakubalika kwani kuna watu ambao wamekuja bungeni lakini hawakuchaguliwa na wananchi.
“Ninyi
waandishi mnajua kuwa uchaguzi ulivyokuwa wapo watu ambao wamekuja
bunge bila kushinda na wengine wametangazwa bila hata kupigiwa kura”. Alisema
“Inafaa
zaidi kama angepatikana spika ambaye hatokani na chama chochote cha
siasa ili kuweza kuondokana na ushabiki wa kulinda maslahi ya chama
fulani.
“Wapo
watu wengi ambao siyo wabunge lakini wanaweza kuendesha vyema bunge
jambo ambalo akipatikana spika toka nje ya bunge anaweza kuendesha bunge
vizuri” alisema Mbowe.
Kauli
ya Mbowe imetokana na Mbunge mteule wa jimbo la Mtera Livingston
Lusinde (CCM) aliyenukuliwa akisema spika lazima awe mbunge.
Lusinde akizungumza na waandishi wa habari alisema kuwa mtu yoyote ambaye anatoka nje hataweza kumpigia kura.
Kwa
upande wake Mbunge mteule wa jimbo la Kisarawe Sulemani Jafo (CCM)
alisema spika ambaye atapatikana ni lazima alisimamie vizuri Bunge.
Amesema wananchi wengi wana matarajio makubwa na bunge kwa maana ya dhana ya mabadiliko.
Mbali
na hilo alisema wabunge wanatakiwa kulitumia Bunge kwa lengo la
kuisimamia selikari kwa lengo la kutetea maslahi mapana ya watanzania
wote bila kujali itikadi za vyama.
“Nataka
kuwaambia wabunge wenzangu hususani vijana wahakikishe wanafanya kazi
ya kuisimamia serikali bila kujali itikadi za vyama vyao na wala
kupingana kama vile wanakomoana.
“Pale penye ukweli ni vyema wabunge wote tukakubaliana kwa nia moja kwa lengo la maslahi mapana ya watanzania wote,” amesema Jafo.
Post a Comment