Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UKAWA wamtangaza Ole Medeye kuwa Mgombea Uspika



Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) umemteua, Goodluck Ole Medeye (Chadema) kusimama katika nafasi ya uspika,huku katika nafasi ya unaibu Spika akiteuliwa,Magdalena Sakaya wa Chama Cha Wananchi (CUF).

Tangu kuanza kwa mchakato wa kumpata mwakilishi aliyekuwa anatazamiwa kuwakilisha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kinyang’anyiro cha nafasi ya uspika Mpekuzi ilibaini kuwa jina la Goodluck Ole Medeye, ndilo lililokuwa likitajwa kuwa litasimamishwa katika nafasi hiyo.

Ole Medeye, aliwahi kuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi kupitia CCM,aliwahi pia kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika utawala wa awamu ya nne wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete (CCM).

Umoja wa Vyama unaofahamika kama Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top