Bernard Paul 'Ben Paul'.
UKIACHANA na
vyombo vya muziki, kingine kinachombeba msanii ni ubora wa sauti yake
na hata akiimba ‘live’ basi ladha yake hupenya zaidi kwenye masikio ya
wasikilizaji. Tanzania tumejaaliwa kuwa na wasanii wazuri wenye sauti
zenye mvuto lakini wengi wao hupotezea sanaa hiyo na kuamua kujikita
katika maisha mengine ya kujitafutia kipato.
Ali Kiba.
Sabau
kubwa inayowaondoa katika muziki ni kukatishwa tamaa na mapromota
wachache wanaojali maslahi yao binafsi na kumuacha msanii akipata
shida.Ukiangalia kwa upande wa ‘mamtoni’, wasanii wamekuwa wakichukulia
muziki kama kazi na ndiyo wanaingiza kiasi kikubwa sana cha fedha.
Mfano
mzuri ni P Diddy, leo hii anamiliki helikopta, boti na vitu vingine
vingi kutokana na muziki.Wale wenye sauti tamu kama Ne-yo, Chris Brown,
Trey Songz na wengineo kibao wamekuwa wakisaidia kutusahaulisha maisha
ya shida kupitia muziki wanaoufanya.
Yote
tisa, kumi msanii bila kufanya kolabo (ushirikiano katika nyimbo) na
wenzako mara nyingi mashabiki wako wanakuwa wanashindwa ‘kujaji’ uwezo
wako.Hapa nakuletea wasanii wa Tanzania ambao ukiwapa kolabo hasa kwenye
kuimba kiitikio hakika hutembea mulemule na wanaweza kumtoa chipukizi
au msanii mgeni kwenye tasni hiyo;
ALI KIBA Anasifika
kwa sauti matata ambayo wengi hupenda kuisikia akiimba ‘live’ kwani
hiyo ‘vocal’ yake ni noumaaaa! Angalia kazi anazoshirikishwa na namna
anavyozitendea haki.Amefanya kolabo nyingi sana na zote amekimbiza na
nyingine kuwafunika kabisa wahusika wakuu wa nyimbo.Baadhi ya ngoma
alizoshirikishwa na kufanya vizuri ni Nai Nai aliompa sapoti Ommy Dimpoz
na kumtambulisha kisanaa, Msambinungwa ya Tundaman hapo bado haijatajwa
Hands Across the World aliofanya na wakali kibao kutoka Afrika na mkali
wa R&B, Robert Kelly wa Marekani. Asilimia kubwa ya ngoma
anazoshirikishwa huwa zina-hit.
BARNABA Elias
Barnabas kijana ana umbo dogo lakini kazi yake ni kubwa sana. Ni zao la
Tanzania House of Talent (THT), amekuwa akitoa sapoti kubwa sana kwa
wenzake.Pia amefanya kazi nyingi sana na ana uwezo wa kufunika vilivyo
kwenye kazi anazoshirikishwa. Amefanya kolabo na Izzo Biznes Ngoma ya
Love Me akiwa na Shaa,Nivute Kwako ya Dayna, Natumaini aliyopewa shavu
na
Beka,
Zamani remix ya Q Chillah na nyingine kibao. Mara nyingi hachagui
kufanya kazi na mtu cha msingi anazingatia kama una kipaji ndipo anakupa
nafasi ya kukubusti kwa kutumia sauti yake.
DULLY SYKES
Jina
lake kamili ni Abdul Abby Sykes, ana umri wa miaka 34, ukitaja kati ya
listi ya wasanii wa Bongo Fleva ambao wamedumu zaidi kwenye sanaa hiyo
basi hutaacha kutaja jina lake. Hii yote ni kutokana na kazi yake
kukubalika na watu wa aina tofauti kuanzia watoto na watu wazima.
Amejitahidi sana kuwaibua wasanii wengi ambao wamepitia kwenye studio
yake ya Dhahabu Records lakini pia jamaa sio mchoyo wa kolabo, ukimpa
nafasi akuimbie kiitikio basi ni lazima akamue na ngoma inafanya vizuri
ikiwa tofauti basi ni mapenzi ya Mungu. Ameshiriki katika Ngoma ya
Action ya C Pwaa akiwa na Ms Trinit na Ngwair, Mdananda wa Shetta,
Manenomaneno wa Queen Darleen na nyingine kibao lakini sasa tazama
nyimbo zake zinavyochana spika mitaani hatari sana!
BEN POL Wazazi
wamempa jina la Bernard Paul Mnyelange, sasa hivi anatesa na Wimbo wa
Sophia, naye ameingia kwenye listi ya wasanii ambao pengine wanafanya
vizuri kila wanaposhirikishwa na wenzake. Alifanikiwa kutwaa Tuzo mbili
za Kili kama Mwimbaji Bora wa R&B 2011-2012 kupitia ngoma zake za
Nikikupata na My Number One Fun. Baadhi ya Ngoma alizoshirikishwa ni
Mama Yeyo ya G Nako, Sitaki Kazi ya Nikki wa Pili, Sikati Tamaa ya
Darasa na
zote amekamua kwenye kolasi na inaonyesha jamaa yupo vizuri kikazi.
G NAKO Jina
lake la kazini anaitwa George Sixtus Mdemu a.k.a G Nako. Nani
asiyemfahamu msanii huyu kwa sasa? Bonge moja la msanii ambaye kolabo
yoyote anakaa, jamaa anatokea Kundi la Weusi na asilimia kubwa amekuwa
akihusika kuimba kolasi za ngoma za kundi hilo. Amefanya nyimbo nyingi
na wasanii wenzake na akatusua kama Mfalme ya Mwana FA, XO ya Joh
Makini, Bum Kubam aliyoshirikishwa na Nikki wa Pili, Tumewaka aliyompa
sapoti Godzilla na nyingine nyingi
Post a Comment