picha
upo eneo tulivu, masikioni umeweka ‘headphones’ na unasikiliza nyimbo
za wakali wa muziki Bongo, unaanza na nyimbo za Juma Musa ‘Jux’ kisha
unafuatia za mkali wa Hip Hop, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’.Hamu inakuwa
haijaisha vizuri kwa upande wa Hip Hop, unaamua kusikiliza nyimbo za
Nickson Simon ‘Nikki wa Pili’ kisha unachukuwa juisi na kumalizia fundo
la mwisho.
Kabla
hujainuka kuondoka eneo hilo, unaamua kusikiliza nyimbo za ‘pacha’ wa
Bongo Fleva, Chegge na Temba lakini kuna kitu kinakupa hasira.Kwa nini
‘hawasongi’ kimataifa? Unavuta tena picha, Jux yupo karibu sana na
Vanessa ‘Vee Money’, Diamond na Chegge na Temba, Mwana FA na AY, Nikki
wa Pili na Joh Makini na wenzao wote wanatambulika kimataifa. Swali
linakujia WAMEROGWA AMA?
Jux na Vee Money
Hakuna asiyekubali uwezo wa Jux katika muziki wa R&B nchini, mkali
huyu anabamba kinoma na ngoma kama vile Sisikii, Nitasubiri, Uzuri Wako
na nyingine nyingi. Amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Vee Money
tangu mwaka 2014. Uhusiano wao ulifika mbali zaidi kwani walikuwa pamoja
katika ‘tour’ mbalimbali ndani ya nchi.
Tangu
mwaka huo 2014 hadi sasa Vee Money ameshashiriki katika tuzo za
kimataifa zaidi ya tatu yaani All Africa Music Awards (Afrima), MTV
Africa Music (MAMA) pamoja na African Muzik Magazine Awards (Afrimma).
Mbali na tuzo hizo, Vee Money ameshapiga shoo kibao za kimataifa akiwa
peke yake (Marekani, Afrika Kusini, Nigeria n.k) ambazo zimemfanya
kujulikana kila kukicha na wanamuziki wa kimataifa. Kwa upande wa Jux,
asilimia kubwa anajulikana ndani ya nchi tu. Hakuna dalili yoyote ya
‘kushikwa mkono’ kimataifa na Vee Money.
Nikki wa Pili na Joh Makini
Ni kati ya ndugu wanaokimbiza katika muziki wa Hip Hop Bongo. Mastaa
hawa wanaunda kundi la Weusi wakiwa na wenzao G Nako pamoja na Bonta.
Katika sherehe ya Zari All White iliyofanyika Mei mwaka huu, staa wa Hip
Hop kutoka ‘Sauz’ AKA alikuwa mmoja wa waalikwa na ujio wake huu
ulimfanya Joh Makini kupata nafasi ya kolabo naye.
bali
na kufanikiwa kolabo hiyo, Joh ameshatoka na Ngoma ya Nusunusu ambayo
kwa mara ya kwanza video yake ameifanyia nchini Afrika Kusini na hivi
sasa yupo mbioni kutoka kimataifa zaidi na staa wa Nigeria, Davido.
Juhudi zote hizo bado hazionekani ‘kumbeba’ Nikki wa Pili kumpeleka
kimataifa.
Diamond vs Chegge na Temba
Haina
mjadala kama Diamond kwa sasa ndiye mwanamuziki anayekubalika zaidi
nchini Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika. Amekuwa akijizolea tuzo
lukuki za kimataifa na hivi karibuni aliweka historia Ulaya kuwa
Mtanzania wa kwanza kuchukua Tuzo ya MTV EMA akimpiku mwanamuziki na
aliyewahi kuwa mrembo wa dunia 2000, Priyanka Chopra kutoka India.
Lakini
nyuma ya pazia, wanaomuongoza Diamond kuelekea mafanikio yake ni haohao
wanaowaongoza Chegge na Temba. Diamond amejizolea heshima kubwa nchini
Nigeria na Sauz lakini juhudi za kuwapeleka kimataifa zaidi Chegge na
Temba hazionekani. Mara ya mwisho pacha hao walifanikiwa kutinga Sauz na
kufanya Ngoma ya Kaunyaka lakini bado haukuwafanya kubamba kimataifa na
hii inaonekana sapoti kutoka kwa Diamond ipo chini.
Mwana FA vs AY
YUPO
kimya lakini akiachia ngoma huwa gumzo kila kona, Ngoma yake ya mwisho
ilikuwa Mfalme ambayo ilikuwa gumzo kutokana na mashairi na kumpelekea
kuibuka na Tuzo za Kili 2015. Muda mrefu FA amekuwa ‘swahiba’ wa AY na
kuna kipindi walijiunga pamoja kama kundi na kufanya muziki kisha kila
mmoja akarudi kufanya muziki kivyake.
Mbali
na kuwa karibu lakini hakuna dalili ya FA kushikwa mkono na AY kufanya
muziki wa kimataifa. AY hadi sasa anashikilia tuzo nyingi za kimataifa
kutoka Channel O, MTV Music (Mama) na ameshafanya shoo kibao za
kimataifa sambamba na kufanya kolabo na mastaa wakubwa duniani kama vile
Sean Kingston, Lil Romeo na wengine kibao. Pia AY ndiye balozi wa
Godfather (kampuni kubwa ya Sauz inayowatengenezea mastaa video za
kimataifa).
Post a Comment