STAA
asiyekaukiwa matukio Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’
amewacharukia watu wanaohoji kwa nini anapendeza angali mwanafunzi kwa
kuwaambia, ‘kwani akiwa mwanafunzi ni mwiko kupendeza?’
Akizungumza
na mwandishi wa habari hii hivi karibuni, Lulu alisema amekuwa akiona
maoni ya watu wengi mtandaoni wakihoji anapata wapi fedha za kupendeza
wakati yeye ni mwanafunzi hoja ambayo ameiona haina mashiko kwani yeye
hatumii fedha nyingi katika urembo wake.
“Watu
bwana! Ningekuwa niko rafu wangesema pia na hata hivi ninavyopendeza
watu wanachonga pia sasa jamani kipi kitu kizuri ili watu wafurahi na
nafsi zao? Mimi umaridadi hapa ndiyo kwake na sijaanza leo, japo sina
fedha lakini kidogo nilichonacho kinaficha umasikini,” alisema Lulu.
Chanzo: GPL
Post a Comment