Rais wa Urusi, Vladimir Putin amepiga marufuku safari ya ndege zote
za Urusi kuelekea nchini Misri hadi pale itakapobainishwa kwa usahihi
sababu zilizopelekea kuangushwa kwa ndege ya nchi hiyo, Metrojet Flight
9268 katika eneo la Sinai, Jumamosi iliyopita.
Uamuzi
huo wa Rais Putin umekuja kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na mkuu wa
kitengo cha huduma za ulinzi za Urusi, Alexander Bortinikov kupitia
kikao cha kamati maalum iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kuanguka kwa
ndege hiyo, kikao kilichorushwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa ya
nchi hiyo.
Urusi imepinga vikali ripoti ya uchunguzi uliofanywa
na Marekani na Uingereza iliyodai kuwa huenda ndege hiyo ilianguka baada
kufuatia kulipuka kwa bomu lilipandishwa kwenye ndege hiyo na mmoja
kati ya wafanyakazi wa ndege hiyo. Ripoti hiyo imeeleza kuwa shambulio
hilo linaweza kuwa la kigaidi kama sehemu ya kupinga uamuzi wa Urusi
kuingiza vikosi vyake nchini Syria kupambana na kundi la ISIS.
Hata hivyo, ripoti hiyo pia ilipingwa vikali na viongozi wa serikali ya Misri.
Post a Comment