Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa michuano ya Kombe la
Shirikisho (AzamHD Federation Cup) utakaofanyika leo Jumatatu, saa 9
kamili mchana katika uwanja wa Karume ambapo timu ya Abajalo FC itacheza
dhidi ya Transit Camp zote za jijini Dar es salaam.
Michuano
hiyo ilianza kutimua vumbi jana kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja
wa Karume uliopo mjini Musoma, ambapo Vill Squad ya jijini Dar es
salaam iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3- 1 dhidi ya timu ya JKT
Rwamkoma ya mkoani Kagera.
Katika
uwanja wa CCM Kirumba, Pamba FC ya jijini humo watakua wenyeji wa timu
ya wachimba dhahabu kutoka mkoani Shinyanga, Bulyanhulu FC mchezo
utakaoza saa 10:30 jioni.
Jumla
ya timu 64 zinashiriki michuano hiyo kutoka Ligi Kuu, Ligi Daraja la
Kwanza na Ligi Daraja la Pili kuwania kutwaa ubingwa, ambapo Bingwa wa
michuano AzamHD Federation Cup atapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye
Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
Post a Comment