Mkuu
wa Dawati la Jinsia katika Kituo cha Polisi Mkoa wa Kipolisi
Chang'ombe, Thecla Kitajo (kulia), akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani), Dar es Salaam leo mchana, ambao wanatembelea vituo vya
polisi na masoko ya Manispaa za Ilala na Temeke kujionea jinsi vitendo
hivyo vilivyo pungua baada ya Shirika la Equality for Growth (EfG) kutoa
mafunzo ya kupinga ukatili huo katika maeneo hayo. Kushoto ni Ofisa wa
Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Meshack Mpwage.
Ofisa wa Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Meshack Mpwage, akizungumza katika mkutano huo.
Ofisa
wa Jeshi la Polisi wa Kituo cha Chang'ombe, Digna Ngatena (kushoto),
akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Mwanasheria wa Shirika la EfG,
Grace Mate)
Maofisa
wa Jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wa Kituo cha Polisi Chang'ombe.
Kutoka kushoto ni Albentina Aloyce, Nuni Munisy na Rose Lukanga.
Dotto Mwaibale
WAKATI
vitendo vya ubakaji na udhalilishaji kwa watu wakubwa vikipungua
matukio ya vitendo hivyo kwa watoto wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es
Salaam vimekuwa vikiongezeka kila siku.
Hayo
yalibainishwa na Mkuu wa Dawati la Jinsia wa Kituo cha Polisi Mkoa wa
Kipolisi Temeke Chang'ombe Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Thecla
Kitajo wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo
mchana, ambao wanafanya ziara katika masoko ya Manispaa ya Ilala na
Temeke na vituo vya polisi kujua vitendo vya ukatili wa kijinsia
ulivyopungua katika maeneo hayo baada ya Shirika la Equality for Growth
(EfG), kutoa mafunzo ya kupinga ukati huo.
"Vitendo
vya ukatili wa kijinsia na ubakaji kwa watu wakubwa umepungua kwa kiasi
fulani lakini kwa upande wa watoto bado tunachangamoto kubwa kwani kila
siku tunapokea kesi ambapo kwa mwezi tunapokea matukio zaizi ya 25 na
zaidi" alisema Kitajo.
Kitajo
alisema hali hiyo inatokana na watoto hao kufanyiwa vitendo hivyo na
watu wazima ambao wengi wao ni jamaa zao wa karibu na tabia ya wazazi
kuwa mbali na watoto wao.
Alisema
licha ya Jeshi la Polisi kujitahidi kufuatilia kesi hizo lakini
zimekuwa zikiishia njiani baada ya wanaotakiwa kutoa ushahidi kushindwa
kufika mahakamani kwa hofu ya watenda kosa ambao ni wapenzi na hao
walifanyiwa vitendo kuja kungwa na sababu za kifamilia.
Alisema
vitendo vya udhalilishaji na ubakaji vitakwisha iwapo tu jamii
itavikataa kwa nguvu moja badala ya kuliachia jeshi la polisi
kuvishughulikia.
Ofisa
wa jeshi hilo wa dawati hilo, Meshack Mpwage alisema umaskini na mambo
mengine kama ya mgeni akifika nyumbani na kulazwa na watoto pia
unachangia kwa kiasi kikubwa watoto kubakwa.
"Wazazi
wamepanga vyumba viwili cha kwao na watoto mgeni akija anapangiwa
kulala na watoto hukuo chumbani mgeni huyo anaamua kuwadhalilisha watoto
au mtoto" alisema Mpwage
Mpwage
alisema tabia ya ubize kwa wazazi pia ni moja ya sababu inayowawafanya
watoto wakikutwa wamekwisha haribika kwa vitendo hivyo kwa sababu ya
wazazi wao kuwa mbali nao na kushindwa kujua kinachoendelea dhidi yao.
Alisema
hivi sasa changamoto kubwa ya watoto ipo kewa madereva taksi ambao
wazazi wanawatumia kuwapeleka mashuleni na madereva bodaboda ambao
uwashawishi watoto hao kwa kuwapa chipsi na fedha chini ya shilingi 1000
na kuanza kufanyanao mapenzi.
Mpwage
alitoa mwito kwa kila mtu kujengea tabia ya kupiga vita vitendo hivyo
vya udhalilishaji kwa kutoa taarifa polisi jambo litakalo saidia
kupunguza vitendo hivyo kama sio kuvimaliza kabisa.
Post a Comment