Ramani rasmi ya Tanzania iliyotolewa na Serikali mwaka 2013
SERIKALI
imesema itavichukulia hatua vyombo vya habari pamoja na watu
watakaobainika kutumia ramani ya Tanzania ambayo sio sahihi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, alisema kumekuwa na matumizi ya ramani
ya Tanzania ambayo inaonesha Ziwa Nyasa lipo katika nchi ya Malawi
pekee huku Tanzania ikionekana kutohusika kabisa katika ziwa hilo.
Mwambene
alisema ramani sahihi ya Tanzania inaonesha Ziwa Nyasa lina mpaka
katikati ambao unaonesha umiliki wa ziwa hilo upo upande waTanzania na
Malawi. Aliongeza kuwa hivi karibuni kumekuwa na vyombo vya habari
ambayo vimekuwa vikitumia ramani hiyo ambayo sio ramani sahihi.
“Ni
vibaya sana vyombo vya habari kutumia ramani ambayo sio sahihi kwani
kufanya hivi ni kuharibu utaifa na utambulisho wetu,” alisema Mwambene.
Post a Comment