Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Bw.
Gerald Mwanilwa akizungumza na Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya
TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy.
Kushoto ni Bw. Slyvester Kibona, Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa
Morogoro. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02
hadi 06 Novemba, 2015.
Mkurugenzi
wa msaidizi (Mafunzo) Bibi Felister Tirutangwa akizungumza wakati wa
mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na
Wizara ya Fedha. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe
02 hadi 06 Novemba, 2015.
Baadhi
ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) na Wizara ya Fedha
wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya program ya TEAMMATE. Mafunzo hayo
yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Mgeni
rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka
NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali, Bibi Wendy Massoy akizungumza na wanahabari kuhusu mafunzo
hayo.
Mgeni
rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka
NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali, Bibi Wendy Massoy akiwa katika picha ya pamoja na watumishi
wanaohudhuria mafunzo hayo.
Mkurugenzi
wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Bw.
Gerald Mwanilwa akizungumza na wanahabari kuhusu mchango wa Serikali ya
Awamu ya Nne katika kuhakikisha uhuru wa CAG unapatikana.
Na Mwandishi wetu, Morogoro
Watumishi
wa umma nchini wenye fani ya ukaguzi, wametakiwa kutumia weledi katika
utendaji kazi zao hali itakayoongeza ufanisi katika usimamizi wa
rasilimali za umma.
Wito
huo umetolewa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,
Bibi Wendy Massoy wakati akifungua mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa
ajili ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Wizara ya Fedha.
Bibi
Massoy amesema, viwango vya ukaguzi Kimataifa vinahitaji mkaguzi
kuhifadhi taarifa zake za ukaguzi vizuri ili kuwezesha mkaguzi mwengine
kuweza kufikia hitimisho moja kulingana na kazi iliyofanywa na Mkaguzi
mwengine.
“Programu
ya TEAMMATE hutoa fursa kwa wakaguzi kwa kuwawezesha kuhifadhi taarifa
zake za ukaguzi vizuri hivyo kuwafanya kutii viwango vya ukaguzi
Kimataifa vya ukaguzi,” alisema Bibi Massoy.
Kaimu
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameongeza kuwa mafunzo
hayo yanalenga kuwajengea uwezo wakaguzi hao katika kazi yao ya ukaguzi.
“Nawasihi
muweze kutumia fursa hii kujiendeleza na kutekeleza utaratibu wa kaguzi
wa mwongozo kwa vile wengi wa hatua na taratibu wamekuwa umeboreshwa
katika Teammate Programu.
Akizungumzia
mchango wa Serikali ya Awamu ya Nne katika kuiboresha Ofisi ya CAG,
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Gerald Mwanilwa alisema
kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imechagizwa na
uamuzi wa dhati wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuimarisha taasisi za
utawala bora, maadili na udhibiti, ikiwemo NAOT.
Bw.
Mwanilwa aliongeza kuwa Rais alifanya hivyo kwa kuboresha sheria,
kuongeza uhuru wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, kuongeza uwazi wa taarifa
za Ofisi hiyo kwa kupeleka Ripoti za CAG kwa mara ya kwanza Bungeni
pamoja na kuboresha mazingira ya kazi.
“Kwa
mara ya kwanza Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliitisha vikao mbalimbali,
kwa nyakati tofauti na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wakuu
wa Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa kusisitiza umuhimu wa
kuzipitia na kuzifanyia kazi taarifa zinazotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali. Hii imeleta mwamko mpya katika kuona
umuhimu wa ripoti hizi na kutumika katika kufanya maamuzi mbalimbali
serikalini,” alisema.
Bw.
Mwanilwa aliongeza Katika Uongozi wa Awamu ya Nne NAOT ilishuhudia
uanzishwaji wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma, ambapo serikali ilitunga
Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya Mwaka 2008 pamoja na kanuni zake za mwaka
2009. Sheria hii iliongeza wigo na uhuru wa Ofisi hii katika kutekeleza
majukumu yake Kikatiba.
Kuhusu
Bajeti ya uendeshaji wa NAOT, Bw. Mwanilwa aliongeza: “Rais Kikwete
aliongeza Bajeti ya Ofisi ya Ukaguzi ambapo Serikali iliboresha
utaratibu na mchakato mzima wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Mdhibiti na
Mkaguzi wa Hesabu za Serikali uliowezesha bajeti ya Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi kuongezeka kwa asilimia 306% katika kipindi cha miaka mitano,
kuanzia mwaka wa fedha wa 2008/9 hadi 2013/14.”
Jumla
ya wakaguzi 65 kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na kutoka 25 Wizara ya
Fedha wanahudhuria mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika mkoani
Morogoro.
Post a Comment