Wanachama
zaidi ya mia moja wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Pangani Mkoani
Tanga wametishia kujeresha kadi zao za chama na kujiunga na vyama
vingine vya siasa..
Madai
ya wanachama hao ni kutaka kurejeshwa kwa jina la aliyekuwa mbunge wa
viti maalumu Amina Mwidau kwa kuwa ndiye aliyeshinda kwenye kura za
maoni na kuliondoa jina na Saumu Sakala aliyeshika nafasi ya pili kwenye
mchakato wa kura za maoni.
Wananchi
wa chama cha wanchi CUF waliokuwa wakitishia kukihama chama hicho
kufuatia kutorejeshwa kwa jina la Aliyekuwa mbunge wa viti Maalumu Amina
Mwidau.
Wanachama
hao wanasema chama hicho kinaweza kufa kama uongozi wa juu hautasikia
kilio hicho chenye maslahi ya kisiasa katika wilaya ya Pangani.
Katubu wa chama hicho wilaya ya Pangani Ramadhan Hadadi amesema waliofanya kazi hiyo ni Baraza la uongozi la chama hicho Taifa.
Amina
Widau licha ya kugombea viti maalumu kupitia chama hicho ,aligombea
kwenye jimbo la Pangani na kuangushwa na mgombea CCM Jumaa Aweso.
Post a Comment